Header Ads

MANISPAA ya Morogoro kwa kushirikiana na Dawati la Kijinsia na Watoto Mkoa wa Morogoro pamoja na Kituo cha msaada wa Kisheria Morogoro washerekea maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia.



HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na Dawati la ukaguzi wa Kijinsia Mkoa wa Polisi wa Morogororo pamoja na Kituo cha Msaada wa Sheria Morogoro wameungana kusherekea maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Novemba 25, 2019 kwenye Viwanja vya Kilakala Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mkuu wa  Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi wa Morogoro, Sophia Ngosso, amesema maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hufanyika kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemaba 12 yakiwa na lengo la kuzungumzia masuala mbali mbali yanayohusu ukatili katika Jamii.

Amesema kwa upande wa Morogoro, wameadhimisha maadhimisho hayo na kwa kutoa elimu pamoja na kuandaa kongamano ikiwamo kucheza mechi kati ya Waendesha Boda boda na Bajaji  kwani lengo la kuwakutanisha ni kutaka kupata ushirikiano baina ya Wananume na Wanawake .

Aidha amesema siku zote wamekuwa wakiegemea kuwapatia elimu Wanawake na Watoto  huku wakiwasahau wanaume ambapo kwa upande wake amesema wanaume ndio kichochezi kikubwa cha ukatili wa Kijinsia katika Jamii.

"Tumeamua kuwakutanisha wanaume hapa kwani tunawasahau sana , ukiangalia katika takwimu yetu wanaume, Dereva wa Boda boda na Bajaji wanaongoza katika kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia, hivyo tumeitana ili tupeane mikakati thabiti na kuwafanya kuwa mabalozi wazuri na kuondoa ukatili huu ndani ya familia na nje ya jamii inayomzunguka " Amesema Bi. Ngosso.

Amesema raia yake baada ya maadhimisho hayo jamii itakuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia, na jamii itaishi huru bila ukatili wa kijinsia huku akisema hawatamvumilia mtu yeyote atakayefanya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wa Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria Mkoa wa Morogoro (Morogoro Paralegal Center), Bi. Joyce Peter, amesema kituo chao  kinashughulika na kutoa elimu dhidi ya ukatili hivyo kwa kongamano hilo ana amini  jamii itaanza kubadilika.

Naye Nahodha wa Timu ya Bod boda, John Luhembe, amesema mafunzo yaliyotolewa yatawasaidia sana hususani katika vikundi vidogo vidogo vya wananchi wataweza kuwa mabalozi wema wa kusimamia misingi ya sheria na kanuni pamoja na kuifuata katiba ya Jamhuri ya Muungano na kuacha tabia ya kufanya vitendo vya ukatili wa Kijinsia.

"Amesema kuwa, sio boda boda wote wanajihusisha na ukatili wa kijinsi lakini wakati mwengine hali hii inatokana n na ugumu wa maisha, kwani unakuta mwanafunzi anatoka nyumbani mzazi hampi pesa ya kula hivyo akiwa anapakiwa na boda boda na kuweza kumlaghai, lakini watakaa na boda boda kwa ajili ya kupeana  elimu kwani inaonekana boda boda wanalalamikiwa sana katika ukatili wa kijinsia kwa Wananfunzi" Amesema Luhembe.


Mkuu wa  Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi wa Morogoro, Sophia Ngosso. 







No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.