MAMIA YA VIJANA WENYE UTAALAMU WA IT WAITIKA WITO WA RC MAKONDA
Mamia ya Vijana wenye utaalamu wa Teknolojia IT* leo *wamefurika* kwa wingi kuitika wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,Mhe. Paul Makonda* aliewahitaji kwajili ya kuandaa Mfumo wa wa Kuratibu uwajibikaji wa wa Watendaji wa Umma* kwa lengo la kushughulikia kero za wananchi.*
Kwa mujibu wa *RC Makonda* Mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko dhidi ya *Watendaji wasiowajibika* kuanzia ngazi ya *Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa* na viongozi Wakuu akiwemo *Mkuu wa mkoa,Katibu tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi, Makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara* Watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiewajibika kutatua *kero za wananchi.*
Mfumo huo unatarajiwa *kuongeza uwajibikaji* kwa watumishi wa umma na kumpa mwananchi *uwezo wa kueleza kero na malalamiko* yake inapotokea amefika ofisi ya umma kuhitaji huduma na watendaji kushindwa kupatia majawabu *kero* zake.
Post a Comment