Header Ads

DC Mjema azindua mradi wa Choo cha kisasa chenye thamani ya Milioni 30 Vingunguti.










MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophi Mjema, Leo amezindua mradi wa choo kipya cha kisasa chenye thamani ya Milioni 30 kata ya Vingunguti.Mradi huo  ni Juhudi za Naibu Meya wa Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti , Omary Kumbilamoto kutafuta wadau wa kusaidiana na Manispaa ya Ilala katika kuiletea maendeleo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Mara baada ya uzinduzi huo, DC Mjema, ameupongeza Uongozi mziwa wa Kampuni ya PMM  kwa jitihada za kuhakikisha wakazi wa Vingunguti wanakuwa na vyoo bora.

 Aidha amesema hiyo ni jitihada ya kuwa na Diwani mwenye  maono ya kutaka  maendeleo kwa wananchi wake kwani ameona Afya ndio kitu cha Msingi katika kuleta maendeleo.

DC Mjema amesema Serikali ya Sasa ina  dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata Vyoo bora nyumbani pamoja na maeneo yao ya mkusanyiko ikiwamo vijiweni, Stendi ya Mabasi  n.k.

Amesema kupata Choo hicho kutasaidia kupunguza magonjwa ya milipuko ikiwamo kipindu  pindu , homa  za matumbo na magjnjwa mengineyo.

Hata hivyo amesema mradi huo unakabidhiwa kwa Manispaa ya Ilala hivyo baada ya makabidhiano hayo kamati itakayoundwa ihakikishe inampata mdhabuni atakayeendesha mradi huo awe na vigezo vinavyostahili ili kufanya kazi hiyo kiufanisi zaidi.

Amewataka wananchi watunze choo hicho na kuhakikisha katika kumpata  mwendeshaji washirikishwe kila hatua ili wapate kujua na kuhoji pale itakapohitajika.

" Huu mradi mzuri sana, nawapongeza PMM kufanikisha huu mradi pia niwasihi wananchi huu mradi muutunze kwani miundombinu ya choo huleta Afya bora hivyo mkifanyia usafi kama kilivyo Sasa utapunguza Magonjwa yaliyopo kwani Magonjwa yote huletwa na uchafu wa Mazingira "Amesema DC Mjema.

Pia amezitaka kamati hizo ziwafikilie watu wenye uhitaji maalumu ikiwamo walemavu , watoto wa shule pamoja na watoto wadogo wanaotembea na Wazazi wao ili kuona kundi hilo linasaidiwa katika kupata huduma hiyo ya Choo.

Ametoa rai kwa Wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto Chooni badala ya kujisaidia hovyo jambo linaloweza kusababisha maambukizano ya maradhi kutoka kwa mtu  mmoja na mwengine huku akimtaka Bibi Afya kuendeleza zoezi la  utozwaji wa faini kwa wale wanaokiuka Sheria na utaratibu.

Amesema lipo gonjwa sugu linalosumbua miradi Mingi kushindwa kufikia malengo na kuleta sintofahamu kwa wananchi katika swala la  usomaji wa mapato na matuminzi hivyo baada ya mradi huo kupata mwendeshaji zoezi hilo lifanyike kwa mujibu wa Sheria na utaratibu.

Choo hicho kilichojengwa na Kampuni ya PMM kina jumla ya matundu 6 na bafu 4 ambapo bafu 2 kwa Wanawake na matundu 3 huku matundu 3 yakiwa upande wa Wanaume na bafu 2.

 Hata hivyo hakuishiria kuzindua choo pekee Bali alikaribisha kero kwa wananchi ambapo kero kubwa ikiwamo ya utozwaji wa Pesa maiti pamoja na ukamatwaji wa boda boda na Polisi usioridhisha huku jibu la  maiti akilitolea maelekezo ya wale wenye hali ngumu waandike Barua wafike ofisini kwake atawasaidia jambo ambalo amesema linawezekana.

 Kuhusu kero ya ukamatwaji wa kutumia nguvu kwa boda boda,  Mratibu Mwandamizi wa Wilaya ya Kipolisi ya Buguruni, Adam Maro, amesema kuwa Habari  za tuhuma juu  ya Jeshi  la   polisi zinazowafikia nyingi  zinakuwa na upotoshaji hivyo inataka ufuatiliaji wa kina kuona kama ni kweli au la. Amesema kwa Sasa atahakikisha anatembea kila maeneo ili kuona changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi.

" Kweli zipo tuhuma kama hizo, lakini makosa mengi hufanya na boda boda wenyewe utakuta mtu  hana leseni, Elementi Sasa ukimkamata analalamika lakini pengine kama ukamatwaji huo upo tuleteeni hayo malalamiko kwa utaratibu tutayafanyia kazi"Amesema Afande Maro.

 Amesema Jeshi  la  Polisi linatumia nguvu pale endapo njia ya kuelimishwa  pamoja na kushawishi zimeshindikana ndipo  ushurutishwaji wa Sheria hutumika.

 Amewaomba wananchi watii Sheria bila shuruti na kupendana ili kujenga Taifa imara lenye usalama na amani katika kujipatia maendeleo.

 Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti , Omary Kumbilamoto , amemshukuru Mkuu wa Wilaya Mh Sophia Mjema kushiriki katika uzinduzi huo lakini pongezi za dhati alizitoa kwa Kampuni ya Mradi wa PMM kusaidia ujenzi wa choo hicho.

 Amesema Mradi wa uboreshaji wa makazi holera  ikiwamo bara bara zote za Mitaa na kata ya Vingunguti mtaa wa Kanga, Majengo , Butiama , Mtakuja wa kujenga vyoo ulianza mwaka 2009.

Amesema mpaka Sasa washajenga vyoo 3   ambapo kila choo kinauwezo wa kuhudumia watu 250 kwa siku kwa bei ya Shilingi 200 hadi 300 kutokana na huduma inayohitajika.

 Hata hivyo amewaomba wasimamizi wasitoe mabomba ya mvua bora wachomoe koki kisha wateja wakiingia wanazifunga kuliko kung'oa kabisa jambo ambalo wakija  wageni ni kwao na nchini hii inayoongozwa na Rais John Magufuli kufikia uchumi wa kati wa Tanzania ya Viwanda.

" Tunakushukuru sana mkuu wetu wa Wilaya anafanya kazi kubwa sana kufikia malengo katika Manispaa hii, tunakuomba usichoke, pia mradi huu Pesa zake zimetolewa na wadau PMM sisi hatujahusika na malipo ya mafundi  hivyo hata uwafikirie  mafundi  wetu Hawa Katika ujenzi wa vyoo vya Mtoto wa kike uwapatie fursa na Vijana wa boda boda wanashughuli yao wamekuomba uwe mgeni rasmi hii ni Bahati kwako kwa kuwa wewe ni mchapa kazi kweli" Amesema Kumbilamoto.

Hata hivyo ametoa shukrani kwa DC Mjema kufanya Manispaa yake kuendeleza rekodi ya ufaulu wa Darasa la  saba kushika nafasi ya NNE katika Manispaa zote Tanzania huku akimuomba awaangalie Wanafunzi 850 waliofaulu  katika Kata hiyo wote  wapangiwe shule ya Sekondari ya Vingunguti ili kupunguza gharama za usafiri kwa Wazazi.

 Mbali na hayo, kwa upande wa Meneja Miradi PMM, Deogratus Chacha, amesema jukumu la  usafi na mazingira ni  la  kila Mtu. Amesema Mji wowote unaokosa miundombinu ya Maji taka na Vyoo haupo Salama . Amesema  PMM wapo tayari kushirikiana na wananchi wenyeji wao walio wakaribisha katika uwekezaji wanakuwa salama kiafya .

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.