Header Ads

Dc Mjema aipongeza Benki ya Barclays kuchochea chachu ya Elimu Manispaa ya Ilala.









MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, ameipongeza Kampuni ya Barclays baada ya kutoa vitabu 5000 kwa Baadhi ya Shule za Msingi Ilala huku akiwa na imani kwamba Sekta ya elimu Manispaa ya Ilala itapanda tofauti na ilipo sasa.

Hayo ameyasema Leo Mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo katika shule ya  Msingi Uhuru Mchanganyiko leo . DC Mjema amesema ugawaji huo wa vitabu utaamsha hali  ya Waalimu kujituma kutokana na uwepo wa vitendea kazi jambo ambalo litapelekea kuongezeka na kupanda kwa ufaulu katika Shule hizo zilizopo ndani ya Manispaa yake.

Amesema vitabu hivyo vitawasaidia watoto hao kwa kila MTU kuwa na kitabu chake cha kujisomea tofauti na ilivyo sasa ambapo Wanafunzi wanakaa makundi kutumia kitabu kimoja. Aidha amesema Ilala ina  idadi kubwa ya Wanafunzi wa shule za Msingi jambo linalopelekea kuwepo na changamoto kubwa ya uhaba wa vitabu.


" Napenda kutoa pongezi kubwa kwa ndugu zetu Barclays kwa kweli wanastahili pongezi kubwa na kuwa mfano wa kuigwa kwa Kampuni nyingine katika kusaidia kuendeleza Sekta ya elimu katika Wilaya yetu na Taifa kwa ujumla, hivyo matumaini  yangu ni kwamba Wanafunzi watosoma kwa bidii na Waalimu watakuwa na hali kubwa ya ufundishaji ili kupata matokeo makubwa tofauti na ilivyo sasa ambapo kitaifa tumeshika nafasi ya 4 katika Manispaa zote nchini  na nafasi ya 2 Kimkoa" Amesema DC Mjema.

 Amewaomba Wanafunzi wavitunze vitabu hivyo ikiwamo kutovichana, kujimilikisha kwa majina kwani sio Mali yao ni Mali ya shule. Pia ametoa rai kwa Waalimu kuwa watinzaji wazuri wa vitabu ili viweze kudumu.

Amesema Serikali ya awamu ya nne , chini ya Rais Magufuli inatoa elimu bure lakini kwa kushirikiana na Wadau kutoa misaada ya Vitendea kazi basi dhana hiyo italifanya Taifa kufanikiwa katika kuelekea uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda.

Naye Mkuu wa Masoko Barclays, Ndugu Aron Luhanga, ameupongeza DC Mjema kwa kuwa karibu nao na jitihada zake za kupambana na Maendeleo ya wilaya yake ikiwamo suala la  Elimu.

 Luhanga amesema kuwa pamoja na kuwa wafanya Biashara lakini wamekuwa wakitoa huduma mbali mbali za kimaendeleo ikiwa  ni pamoja na kuchangia uwezeshaji katika Sekta ya Elimu hapa nchini kama vile kuwasaidia Wanafunzi wa vyuo kumaliza elimu zao vizuri kwa kuwawezesha.

" Tunashukuru sana DC Mjema, huyu ni mama Mpambanaji ndio maana tumeona tumuunge mkono katika Wilaya yake ikiwa ni projekti yetu ya kwanza  kwanza hapa nchini  kutoa msaada wa Vitabu, matumaini  yetu ni kwamba tutaendelea kutoa misaada kadri itakavyo wezekana na tupo tayari kuunga mkono Juhudi zote zinazofanywa na Mh: Sophia Mjema hapa Ilala " . amesema Luhanga.

Katika upande mwengine, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yange Yange, Abraham Gabriel amemshukuru Kampuni ya Barclays  kutoa msaada huo huku akisema  watajitahidi kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kuongoza Kiwilaya.

Pia amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema kwa kuwa kiongozi wa mstari wa mbele katika kuleta Maendeleo Ilala pamoja na kukuza Sekta ya Elimu katika Manispaa yake kwa kuwaunganisha wadau wa Maendeleo na Waalimu .

 " DC Mjema ni mama mchapakazi hakika tumepata jembe anafanya kazi kweli kweli anatuunganisha na wadau shida zetu za kitaaluma zinapungua a kushirikiana vema na Watendaji wake Wilaya akiwemo katibu Tawala na Manispaa  pia pongezi kubwa kwa Rais Magufuli kwa elimu bure na kutuletea jembe Wilayani kwetu" Amesema Mwalimu Gabriel .

Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na Uongozi wa juu Manispaa ambapo Afisa Habari Manispaa Tabu Shaibu akimwakilisha Mkurugenzi pamoja na Katibu Tawala Ilala, Sheila Edward Lukuba, Afisa Tarafa Ukonga, Nikodemas Shirima akimwakilisha Afisa Tarafa Kariakoo Bibi Christina.

Miongoni Mwa Shule za Msingi  zilizopatiwa misaada  ni pamoja na Shule Uhuru Mchanganyiko, Shule ya Msingi Yange Yange, Shule ya Msingi Kiyombo, Shule ya Msingi Mafanikio na Shule ya Msingi Gogo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.