Header Ads

DAS Ilala atoa zawadi kwa Kituo cha kulelea Watoto Msimbazi Center.




















 KATIBU Tawala Wilaya ya Ilala, Sheila Edward, ametoa zawadi katika Kituo cha kulelea watoto pamoja na Wazee kilichopo Kata ya Mchikichini , Msimbazi center Ilala Jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo fupi ya utoaji wa zawadi mbali mbali  kwa Makundi yenye uhitaji maalumu imeandaliwa na Jumuiya ya wanavikundi wa VICOBA chini ya shirika la SEDIT DSM kwa kushirikiana na DAS wa Ilala kwa kufanya  usafi Hospitali ya Amana.

Katika utoaji huo wa  zawadi, liliambatana na zoezi la usafi pamoja na kutembelea Kituo cha Watoto Msimbazi center kinachomilikiwa na Kanisa  Katoriki Jimbo kuu la  Dar es Salaam na  kituo cha kulelea Wazee.

 Hata hivyo kabla ya kuelekea katika utoaji wa zawadi , DAS alipata wasaa wa kujumuika na Wanachama wa SEDIT VIKOBA pamoja na dhehebu la  Kiislamu la  Maura  katika kufanya usafi wa kusafisha bara bara  ya ndani ya  Hospitali ya Amana.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, DAS amemshukuru Juhudi za Shirika la  SEDIT kwa kuviunganisha VIKOBA nchini na kuvilea.

Ametoa shukrani za kipekee za kuanzisha Wiki ya Vikoba na kuonyesha moyo wa namna  ya pekee ya kutoa misaada mbali mbali ikiwa  ni kurejesha fadhila kwa  Jamii.

Amesema lengo la  kufanya Wiki hiyo ya Vikoba ni kukutana na kubadilishana fikra , ambapo kukutana huko kutasaidia kupata majawabu mbali mbali kama vile kujenga nyumba, kusomesha na Biashara kupitia VIKOBA.

Amesema kitendo cha kujitolea kuwasaidia watoto hao kina leta  faraja katika kuona wao ni sehemu moja wapo inayojaliwa na jamii kama watu wengine.

 Aidha amesema kila jamii lazima ihakikishe inawajili watoto pamoja na Wazee kwa kutoa kile  walichonacho katika kuendesha maisha yao.

Amewapongeza sana SEDIT VIKOBA kuwa watu wakipekee na mfano huo unatakiwa  kuigwa na Mashirika mengine ya VIKOBA hapa nchini.

" Nimefarijika sana sijawahi fikiria kwamba  Shirika kama hili lisilo la kiserikali litafanya jambo kubwa kama hili, nitoe rai kwa Mashirika mengine waige kwa kutoa gawio la  faida Katika kusaidia huduma za kijamii katika makundi maalumu " Amesema DAS.

 Hata hivyo DAS ametoa salamu za Mkuu wa Wilaya akisema  angependa kujumuika nao lakini muingiliano wa shughuli za kiutendaji zimesababisha kushindwa kufika Katika hafla hiyo fupi ya maadhimisho ya Wiki ya VIKOBA.

 Amewataka Masisters kutokata tamaa katika kuwalea watoto hao pamoja na Wazee kwani malipo yake yapo kwa Mungu.

Naye Diwani wa kata ya Ilala, Saady Khimji , amesema Jamii iamke kuwasaidia watu wenye uhitaji maalumu kwani kwa kufanya hivyo watasaidia kurahisisha huduma za malezi kupitia kwa Wafadhili waliojitokeza kuwalea watoto na Wazee ukizingatia hali ya maisha imebadilika kila mtu  awe msaada kwa wengine.

 " Sisi kama Serikali tumeona kuna haja ya kutoa elimu kwa jamii juu  ya kuchangia misaada kwa watu wenye uhitaji maalumu, hivyo baada ya zoezi hili tunaziomba Taasisi za Serikali na za Watu binafsi tuige mfano wa SEDIT ulichobarikiwa tutoe hata kama kidogo itasaidia huduma nyingine " Amesema Khimji.

Kwa upande wa Mwanzilishi wa SEDIT VIKOBA, ndugu : George Swevetta, amesema wiki hiyo ya VIKOBA kitaifa inafanyika Jijini Dodoma makao makuu ya Tanzania.

Amesema zoezi la  ugawaji zawadi kwa Vituo vya kulelea watoto lilianzia Kituo cha Mwenge Jana Novemba 5, 2018 ili kurahisisha mzunguko wa safari . Amesema kuwa katika Shirika linalotoa Mafunzo ya VIKOBA kwa uhalisia ni SEDIT.

Ameomba Serikali kupitia upya mfumo wa VIKOBA kwani moja ya changamoto ni ukosefu wa Sheria zinazounda mfumo huo wa VIKOBA hapa nchini.

 " Vikundi hivi havipewi kipaumbele katika mfumo wa kisheria hii yote ni kukosekana kwa mpangilio maalumu na mfumo wa kutoutambua hapo ndiyo kimbilio la  kupambana na umasikini " Amesema Swevetta.

Naye Mkuu wa Kituo cha kulea  Wazee , Sista Luisa Leonard , amesema moja ya changamoto kubwa ni pamoja na ukosefu wa usafiri kwa Wagonjwa wanapozidiwa kuwapeleka Hospitali.

Pia amesema Wazee hao wanakosa huduma ya Habari hivyo wameomba wapatiwe TV na Kinga'amuzi ili kupata taarifa mbali mbali za Habari katika kuona ilani inavyotekelezwa chini ya Rais John Magufuli.

 Hata hivyo katika Kituo hicho walipatwa na Msiba wa Mzee mmoja lakini changamoto kubwa ni kukosekana kwa nauli.

Katika kuona suala hilo la  kusafirisha mwili wa marehemu linafanikiwa, DAS aliamua ifanyike harambee na kupatikana kiasi cha Shilingi Elfu hamsini na tano 55000 ambapo Pesa hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo hicho. Katika hatua nyingine, Sista Luisa amemshukuru DAS kwa fikra zake za kuanzisha harambee na hatimaye imewasaidia kutatua changamoto ya Usafishaji wa mwili wa marehemu. Miongoni Mwa zawadi zilizotolewa na DAS pamoja na SEDIT ni pamoja na Pampasi za watoto mifuko 4 Katika ujazo wa dazeni, maziwa ya Nitrogen kopo 3, Mafita ya kupaka, Mafuta ya kula ndoo moja kubwa, Katoni 4 za Maji makubwa, Blenda ya kusagia juisi, majani ya chai, Maji katoni 4 ndogo, Sabuni ya unga ndoo ndogo , Maharage kilo 22, Sembe unga kilo 25 na Mchele kilo 50.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.