Header Ads

Mh: Mavunde afungua Mafunzo ya kimkakati kwa Viongozi Watendaji wa UVCCM






*Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye ulemavu  Mhe Anthony Mavunde amefunga Mafunzo ya Kimkakati kwa Viongozi na Watendaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi leo jijini Dodoma.*

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ndg Mavunde ameupongeza Umoja wa Vijana wa CCM unaoongozwa na Mwenyekiti Comred Kheri D James na Kusema Uvccm ya Sasa ina Dira imebadilika na inasemwa Vizuri sana na Vijana.

Mhe Mavunde ameeleza juu ya kazi kubwa ya Uvccm kuwa ndio jumuiya yenye dhamana ya kushughulika na kero zote zinazowalenga Vijana.

Amesema *"Uvccm ipo kwa ajili ya kushughulika na kero zote zinazowakabili vijana hivyo lazima kama jumuiya muendelee kuweka nguvu katika kuzishughulikia kero na changamoto zinazowakabili Vijana kote kwanzia ngazi za chini"*

Pia amewataka Viongozi hao waliopata Mafunzo hayo wakayatumie mafunzo hayo kuwa mabalozi bora kwa kupeleka Ujuzi huo kwa Viongozo wote kwanzia ngazi ya chini.

Mhe Mavunde ameelezea juu ya Changamoto ya Vijana wengi katika nchi yetu ya kukosa ajira na kuelezea kuwa *"Serikali imeamua kuwaweka Vijana katika mfumo rasmi kwa maana ya vikundi, makampuni na Saccos na kuwapatia elimi mbalimbali ya namna ya kukopesheka na kujiendesha ambapo mpaka sasa tumepata makampuni ya Vijana zaidi ya 22"*


Aidha amesema *"Ofisi ya waziri Mkuu Imekuja na program ya miaka mitano inayoitwa program ya kukuza ujuzi nchini ambayo inalenga kuwafikia vijana Milioni 4.4 hadi ifikapo mwaka 2021".*

Awali kabla ya Kufunga mafunzo hayo Mhe Mbunge wa Jimbo la Nyamagana   *Angelina Mabula* pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana na Vijana *Mhe Zainabu Katimba* pamoja na Mhe *Maria Kangoye* walizungumza na Viongozi hao na kuwapa nasaha na mafunzo mbali mbali .

*#TukutaneKazini*

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.