Header Ads

U.W.T.Buguruni Mivinjeni wazindua Vikundi vya Ujasiriamali.








UMOJA wa Wanawake Tanzania Kata ya Buguruni Mtaa wa Mivinjeni Leo wamezindua rasmi Vikundi 4 vya ujasiriamali ikiwa  ni maadhimisho ya kuelekea katika uzinduzi wa Jukwaa Wilaya ya Ilala utakaozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema Viwanja  vya Mnazi Mmoja.

Katika uzinduzi huo uliofanyika Leo, mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Barua Mwakilanga. Akizungumza Mara baada ya uzinduzi huo, Mh: Barua Mwakilanga, amesema ili Vikundi hivyo vipige hatua vinahitaji kuwa na masoko ya uhakika.

Hivyo amesema atashirikiana na U.W T kuhakikisha wanapata masoko ndani na nje ikiwa  ni pamoja na kuwaletea Waalimu wenye taaluma ya Ujasiriamali katika kuboresha bidhaa zao na kuwaletea maendeleo.

 " Masoko ndio kila kitu, kama tutakosa masoko hata faida tutaikosa pia na tafsiri yake ni kwamba Vikundi hivi vitakufa na kutofikia malengo tuliyojiwekea, niwaahidi kwamba tupo pamoja kama ninavyojitolea katika chama hata hili nitafanikisha wadau ninao kikubwa ushirikiano wenu na kuniunga mkono" Amesema Mwakilanga.

 Amesema Serikali hii ya awamu ya tano inawapenda Wajasiriamali hivyo imejipanga katika kuhakikisha inawainua kiuchumi na kupiga vita dhidi ya umasikini katika kulifanya Taifa hili kwenda kwenye uchumi wa kati.

 Katika hatua nyingine, Mwakilanga, amewataka U.W.T kuongeza  wingi wa Wanachama kwani waliopo 252 ni wachache hivyo kila ngazi ifanye kazi ya kuongea idadi hiyo ili kupata zaidi ya Wanachama 500 huku akiwaahidi zawadi endapo kazi hiyo itafanyika kwa ufanisi.

 " Huu ni mwisho wangu wa madaraka mwakani mwezi 6 tunawaachia mtaa wenu Sasa ni fursa kunitumia nikiwa bado na utawala, ili kubakiza dola Mivinjeni lazima tuongeze  Wanachama katika ngazi zote na kuwasaidia Matawi mengine kushika dola ili kuleta ushindi mkubwa" Ameongeza Mwakilanga.


Hata hivyo amesema ni yeye hafanyi kampeni kama watu wanavyodhani Bali analipa fadhila kwa kuhangaika na U.W.T kwa kuwa wao ndio walichangia kwa kiasi kikubwa kumuweka madarakani huku akiwataka watu waache siasa uchwara na kufanya kazi kwani muda wa kampeni haujafika na unataratibu zake.

 Aidha amewataka wana CCM washikamane na kupendana na kuacha tabia ya kutupiana Maneno jambo ambalo linasababisha makundi na kuvunja nguvu ya chama. Katika kuhakikisha wajasiriamali hao wapo salama ameahidi kuwapatia Pampu ya Maji na kuwapatia eneo kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga ikiwa  ni ombi la  risala ya kutaka Mradi wa kuwaingizia kipato.

 Amesema hayupo tayari kukabidhi dola kwa upinzani kwani amefanya mengi na hataki kuharibu historia yake  aliyojijengea katika mtaa wake ndani ya madaraka aliyonayo. Amesema ipo  haja ya kuonyesha utofauti  wa dola ikishikwa na chama Tawala na upinzani hivyo kwa nafasi yake anataka kuona CCM inaibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi Mdogo wa  Wenyeviti wa Mitaa 2019  na uchaguzi mkubwa 2020.

Amewataka U.W.T kutafuta eneo zuri ili wajenge sehemu ya kufanyia kazi huku akiahidi kuwasaidia Matofali 500 kama alivyofanya katika kutoa msaada wa Bati 30 katika ujenzi wa Ofisi ya Chama ili Uongozi wake usisahaulike akiwa nje ya madaraka.

Amesema katika upande wa kuboresha michezo, atatoa vifaa  hivyo lakini mpaka pale atakapoona watu wapo Uwanjani  kwani kuna baadhi ya watu sio waaminifu wa Mali za Umma.

Naye Mwenyekiti wa U.W.T Kata ya Buguruni, Bibi Kibini Kabanja ameushukuru Uongozi wa U.W .T Buguruni Mivinjeni kwa kuandaa maandamano hayo kwani hilo ni somo kwa wengine. Amewataka wakina mama waunge mkono Ujasiriamali ili kufikia katika uchumi wa kati.

 " Nimefarijika sana hii ndiyo mbinu bora ya kuondokana na umasikini, wakina mama fursa hii ni adimu sana tuna mwakilishi wetu DC Mjema mpambanaji kweli tuitumie fursa hii kwani ni moja ya Viwanda Vidogo  katika kufikia Sera ya Tanzania ya Viwanda" Amesema Bibi Kabanja.

Amevitaka Vikundi vyote visajiliwe Jiji katika kupata fursa ya kujitangaza.  Ametaka umoja huo uwe mkubwa na kufanya kata mzima kuwa na Vikundi na kuhamasisha Novemba 16 , 2018 wajitokeze kwa wingi Viwanja vya Mnazi Mmoja  kutangaza  bidhaa zao.

Kwa upande wa Katibu wa U.W.T Mivinjeni, Amina Shabani amesema huu ni mwanzo na wanatarajia kuongeza Vikundi vingine. Ameupongeza Mh: Mwakilanga kuutika wito huku akimtaka asichoke kuwasaidia.

Hivyo amemuomba DC Mjema kuwapatia usajili rasmi wajasiriamali ili wafanye kazi zao vizuri.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.