DC KATAMBI AWACHANA VIJANA WANAOCHAGUA KAZI, ATOA AJIRA HII
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amewataka vijana wilayani humo kuacha kukaa kijiweni na kulalamika ukosefu wa ajira ilihali wanachagua kazi.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ipala,DC Katambi amesema fursa za kibiashara zimekua zikiongezeka siku hadi siku yangu Rais John Magufuli atangaze Dodoma kuwa jiji.
Amesema Dodoma imefunguka kwa fursa huku akitolea mfano wa mahoteli ambayo sasa yanafurika wateja huku akiwashauri wananchi hao kufanya biashara ya Kuku kwa ajili ya kuuza kwenye mahoteli.
“ Umaskini tunaukaribisha wenyewe kwa sababu hatutaki kujiwezesha, Serikali inatengeneza mazingira wezeshi, ikiwemo kuitangaza Dodoma kuwa Jiji, hivyo niwasihi vijana wenzangu kuamka na kukimbilia fursa zilipo,” amesema Katambi.
Mkuu huyo wa Wilaya pia aliwataka vijana kujitokeza kuomba mikopo katika vikundi vikundi huku pia akigawa ajira ya papo kwa hapo kwa mmoja wa vijana ambaye ni fundi ujenzi.
“ Juzi nimefunga mafunzo ya mgambo hakuna aliejitokeza, ukitoka mgambo tayari jiji moja kwa moja linakuchukua wewe tunakutumia kama askari kukamata wanaokwepa kodi.
“ Ukikamata mkwepa Kodi unaingiza Sh 30,000 hadi 50,000 kwa siku, lakini nyie hamjitokezi mnachagua kazi za kufanya, ondokeni majumbani muache kuwa tegemezi kwa wazazi,” amesema Katambi.
Hivi karibuni DC Katambi alipofunga mafunzo hayo ya mgambo alisaidia upatikanaji wa ajira 96 za wahitimu wa mafunzo hayo ambapo makampuni ya Ulinzi yaliahidi mbele yake kutoa ajira hizo.
Ameongeza kuwa itakua raha yake kuona kuwa akiandika andiko LA kuomba msaada ukaletwa akiwa bado Mkuu wa Wilaya hiyo.
“ Simnajua Mzee? Mwenye cheo chake? Kakishikilia mkononi hapa ukizingua anakupuliza tu hivi,. Rais hataki mchezo anataka wananchi wahudumiwe, kwahiyo ndugu yangu tushirikiane kufanya kazi bila kuchagua kama kweli tunapenda maendeleo,” amesema Katambi.
Katika hatua nyingine DC Katambi ameahidi kumsaidia mtoto ambaye ana ulemavu wa miguu, macho na mdomo huku akiagiza viongozi wa kata hiyo wanafuatilia maendeleo yake.
Mtoto huyo anaishi na Bibi yake baada ya Baba yake kumkimbia huku akimuita msukule.
“ Baba yake si yupo na anajulikana? Mtendaji na Diwani naomba mfuatilie maendeleo ya huyu mtoto tuone jinsi ya kumsaidia, na huyo Baba yake akamatwe afikishwe mbele ya sheria huku tukiangalia namna gani nzuri ya kumsaidia,” amesema DC Katambi.
Post a Comment