Header Ads

Mkurugenzi Manispaa ya Ilala aomba wadau kuchangia ujenzi wa Vyoo Shuleni


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri ( kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano wa Baraza la  Madiwani Leo ( kulia) ni Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Sheila Edward Lukuba akifuatilia kwa makini mjadala huo( PICHA NA MTANDAO).

MKURUGENZI  wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala JUMANNE SHAURI, amewaomba wadau wanaoweza kuchangia Ukarabati wa Miundombinu Pamoja na Ujenzi wa Vyoo, madarasa katika Shule za Manispaa hiyo kujitokeza  ili kuupunguza tatizo la uhaba wa Vyoo Pamoja na madarasa katika Shule.

Akizungumza Leo  ,katika kikao Cha Baraza la Madiwani ,Amesema wanatazimia kujenga madarasa 500 katika Shule zote Msingi na Sekondari Hadi kufikia June, mwaka 2019.
"Niwaombe Madiwani Kama Kuna wadau mnaowafahamu mnaweza kutusaidia kwa kuwaambia na kuwahamasisha kuchangia Ujenzi wa vyoo Pamoja na madarasa kwani Ni Aibu kwa Manispaa yetu Shule kukosa vyoo au kuwa na matundu machache ya vyoo" Amesema Mkurugenzi.

Amesema katika Shule zenye uhitaji mkubwa wa Miundombinu zitapewa kipaumbele ili kuondoa changamoto zinazokabili Shule hizo ambapo Ni adha kwa Wanafunzi na kupelekea kutosoma vyema.

Amesema katika bajeti waliyoianda wataweza kujenga takribani vyoo 200, ambapo ametoa Rai kwa Wadau kujitokeza kwa wingi kuweza kuchangia Ujenzi wa vyoo ili kuondoa aibu hiyo katika halmashauri.

Aidha amesema Kuna mdau ambaye amejitokeza na amehidi kutoa mabati zaidi ya 100, hivyo wataanza na kukarabati Shule ya Msingi Tabata ambapo Diwani wa kata hiyo amewasilisha Kero kuwa Wanafunzi wanapata adha kutokana na uchakavu wa mabati hayo.


Akiwasilisha Kero hiyo Diwani wa Kata ya Tabata Patrick Assenga amesema ameshafanya Ukarabati katika Shule hiyo,kwa kupiga rangi majengo ya madarasa lakini changamoto imebaki katika uchakavu wa mabati Jambo linalopelea wakati ya mvua Wanafunzi kushindwa kufika shuleni.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.