Mkurugenzi ilala awataka Wafanya Biashara kujifunza kulipa kodi kuelekea uchumi wa Viwanda
Mkurungenzi wa Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam, JUMANNE SHAURI amewataka wafanyabiashara wote kuhakikisha wanalipa Kodi na kufuata taratibu zote za biashara ikiwemo kupata leseni za biashara zao ili kuondokana na adha za kulipa faini.
Akizungumza Leo na waandishi wa habari Katika Ziara ya kukagua maeneo ya biashara Kata ya Buguruni amesema lengo Ni kuwabaini wale wote wanaokwepa Kodi.
Amesema atahakikisha Kila mfanyabiashara anakuwa na lesini Pamoja na kulipa Kodi Kwani Wapo wafanyabiashara wenye maduka makubwa wanakwepa kulipa na wengine wanalipa ndogo kuliko Kipato wanachoingiza.
Amesema wafanyabiashara wengi wanakwepa Kodi, hivyo Katika Ziara amesaini baadhi yao wanakimbilia na kuziacha biashara Jambo linalopelea kufungwa kwa eneo la biashara.
“Tukibaini kuna mfanya biashara anafanya biasharia bila kuwa na Leseni Hatua tunazochukua ni kutozwa faini ya kuanzia shilingi 100,000 , hivyo ni bora kila mmoja anayefahamu kuwa leseni yake imeisha muda wake ama hana ahakikishe anafuata taratibu zote kwani zoezi hili ni endelevu"Amesema Shauri.
Amesema katika ziara hiyo wameweza kubaini wafanyabiashara wengi wanaokwepa kulipa kodi, na wengine kufanya usmdanganyifu, na Hali hiyo imejidgihirisha baada ya wafanya bishara kuyakimbia maduka yao baada ya kuona Ukaguzi.
“Badala ya wafanyabishara kukimbia ni vyema wakaenda Manispaa na TRA ili kuweza kulipa kodi waweze kufanya biashara bila ya usumbufu wowote” alisema.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara ambao maduka yao yamekaguliwa, wamemwomba Mkurugenzi kupunguza ucheleweshaji wa Leseni Jambo linalopelea kukata tamaa ya kufuatilia.
Aidha Shauri Amesema, watahakikisha wanatoa Elimu kwa wafanyabiashara ili kutoa Elimu kwa watu wote, ambao hawafahamu maana na umuhimu was kulipa Kodi.
Pia ametoa with kwa wafanyabiashara wote wa Manispaa hiyo kulipa Kodi Kwani wanapofanya hivyo wanakuza pato la taifa na kuwezesha huduma nyingine kufanyika ikiwemo kujenga Miundombinu ya Shule, Barabara, Hospitali na huduma nyingine za kijamiii na kuweza kufikia uchumi wa Kati ambao Ni wa Viwanda.

Katika Ziara hiyo Mkurungenzi wa Ilala Jumanne Shauri ameweza kutembelea maduka ya biashara mbalimbali Pamoja na viwanda Katika kata ya Buguruni .
Post a Comment