Header Ads

DAS Ilala atoa pendekezo la Elimu ya lishe kuingizwa kwenye Mitaala ya Shule.






KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ilala, Sheila Edward, ameiomba Wizara ya Elimu kuangalia upya mitaala yake na kuona haja ya kuingiza elimu ya lishe ili Wanafunzi wajifunze wakiwa  Watoto.

Hayo ameyasema Leo kwenye Kufunga  Kikao cha semina ya Mafunzo ya kupanga mipango na bajeti ya Lishe Mkoa wa Dar es Salaam.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari, DAS amesema Elimu ya Lishe haijapewa umuhimu mkubwa katika nchi yetu pia wataalamu ni wachache kama Wizara ingeingiza kayika Mitaala ingeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ma kufanua wigo wa uelewa kwa Wanafunzi Shuleni.

 Aidha, amesema zoezi hilo sio la  wataalamu peke bali  Wazazi wanayo nafasi ya kutoa elimu Shirikishi kwa watoto wao. Amesema Serikali ya awamu ya tano imekuja na mpango wa elimu bure , lakini Watoto hawawezi kufanya vizuri kwenye masomo yao bila ya kuwa na Lishe bora.

Hivyo amesema Ofisi ya Wilaya ya Ilala chini ya Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala watahakikisha Pesa iliyotengwa inapatikana kwa wakati. Pia amewataka Wataalamu kutoa matumizi kwa wakati pindi  watakapo ingiziwa hizo Pesa na kuacha tabia ya udanganyifu wa taarifa .

 " Tumefarijika kusaini mkataba huu wa lishe hakika tunaenda kutengeneza vizazi bora kabisa, Watoto wetu wakiwa na Afya bora hata uelewa wao wa masomo itakuwa mzuri, hivyo kama mlivyomsikia Mkurugenzi amesema Pesa ipo  basi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya tupo bega kwa bega na Manispaa kufanikisha hiyo Pesa kwa haraka ili zianze kutumika , nitoe rai taarifa zitolewe kwa haraka na wale wenye tabia ya udanganyifu tukiwagundua tutawachukulia hatua za kisheria" Amesema DAS.

 Kuhusu suala la  posho, amewataka Watendaji kutokufikiria hilo swala badala yake wachape kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli kwa kuishi na  kauli ya hapa kazi tu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.