DC Mjema amuagiza OCD kufuta Vikundi vya boda boda visivyo pitia Mafunzo ya usalama bara barani.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amemuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, OCD Adam Maro, kuvifuta Vikundi vyote ambavyo havitaki kuhudhuria Mafunzo ya Uendeshaji salama wa bara bara katika Wilaya yake.
Hayo ameyazungumza Leo kwenye Ukumbi wa Itigi uliopo Kata ya Vingunguti Mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya ugawaji Vyeti kwa Wahitimu wa Umoja wa Madereva Boda boda Vingunguti ( UMBV).
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo, DC Mjema, amesema chanzo kikubwa cha ajari za boda boda zinatokana na baadhi ya madereva kutokujua Sheria na kanuni bara barani hivyo semina hizo za Mafunzo zinasaidia sana kupunguza wimbi la ajari.
Amesema kuwa kama Vikundi hivyo vikikubali kufanya Mafunzo hayo hata ajari zitapungua
Amesema Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imejidhatiti kuhakikisha Boda boda wanafahamika na kuwaingiza katika utaratibu kama ilivyo kwa ajira nyingine.
" Sisi sio kama tunawachukuia, ila wapo baadhi yenu wanawachafua , Serikali ya Sasa pamoja Manispaa zote hapa nchini Zimejipanga kuona inatatua wimbi la ajari kwa kuanzisha masomo haya hivyo tunaomba Vikundi vyote vihudhurie kwani Kesho letu la Polisi linajitoa sana kushirikiana na nyinyi na wale ambao wataona utaratibu huu ni mbaya kwao waache kazi hoyo Mara moja" Amesema DC Mjema.
Aidha amesema baada ya Mafunzo hayo moja ya faida kubwa yatasaidia Ku wafanya wawe guru katika kazi zao hata inapotokea kazi za dharura usiku wa manane wakiwa na vyeti vyao itakuwa rahisi kwao kwa vile Jeshi la Polisi linawatambua.
Pia amesema furaha yake ni kutaka kuona Boda boda wa Ilala wanakuwa tofauti na wengine.
Aidha amesema jukumu lake kubwa wakati anaingia Wilaya ya Ilala ilikuwa ni kuhakikisha kwamba Vijana wote wanakuwa na shughuli za kufanya aidha kwa kujiajiri au kuajiriwa.
Hivyo amefurahi kuona Ilala inabadilika kadri siku zinavyokwenda huku akiupongeza Uongozi wa Rais Magufuli kwa kuwajali wanyonge na masikini.
Amewataka Vijana kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli kwakuwa wahanga wa kubwa wa ajira katika nchi hii ni Vijana .
Ameupongeza Uongozi wa Boda boda Vingunguti kwa kumaliza masomo yao salama huku akisema Mafunzo hayo yawe na faida ili kuweza kuepuka na ajari bara barani kwa kuzingatia Sheria na kanuni za usalama bara barani.
Amesema huu ni wakati wa Boda boda kunufaika na wakiwa pamoja itasaidia sana kupunguza wimbi la uharifu hapa nchini.
Mbali na hayo , amesema semina za Mafunzo ya utoaji wa mikopo umefanyika kilichobakia ni utendaji tu. Pia amewataka boda Boda hao baada ya kupatiwa mikopo wahakikishe Pesa hizo zinarudishwa kwa haraka.
" Hizo sio Pesa za kula ni Pesa kwa ajili ya kuzungusha katika mitaji yenu, Pesa za Mh: Rais ni za moto hakikisheni muda ukifika fanyeni marejesho fasta ili wengine wapatiwe na kama utashindwa tutatumia njia yoyote mpaka urudishe kwani Pesa hizo zinatolewa kwa utaratibu " Ameongeza DC Mjema.
Pia amewataka boda Boda hao kujiandikisha Katika fursa mbali mbali zikiwamo mifuko ya kilimo, uvuvi pamoja na madini kwani mifuko 19 imeorozeshwa kwa ajili ya Watanzania wote.
Katika kuona boda boda hao wanatambuliwa atahakikisha wanaingizwa katika Taarifa za msingi za kumbu kumbu ( Data base ) ili Manispaa iwatambue kama ilivyo kwa Wamachinga kwa kupatiwa Boma ya Afya, pamoja na T.R.A kwa ajili ya kuingizia Halmashauri mapato.
Amesema kiu yake kubwa ni kuona kila MTU anamiliki boda boda na sio kumfanyia MTU kazi kadri atakavyoendelea anunue Maroli na kuwaachia Boda boda wadogo zao.
Amewataka wananchi wa Vingunguti haswa wakina mama kuchangamkia fursa ya uzoaji taka na fursa nyingine zilizopo Manispaa kikubwa wao waende Manispaa watapatiwa utaratibu kwani wenzao Temeke wameshaanza .
Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Mh: Omary Kumbilamoto, ameupongeza DC Mjema kwa kuwa karibu na Wananchi wake.
Amesema jitihada zake za kutatua kero zimepelekea Shule zake mbili ikiwamo Shule ya Msingi, Kombi kuingiziwa Milioni 20 pamoja na shule ya Msingi Mtakuja Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya ukarabati.
Pia amesema DC Mjema ndiye mtu pekee aliyekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anawasukuma TARURA kukarabati bara bara ya Vingunguti iliyoonekana kuwa mbovu.
Aidha ameupongeza Rais Magufuli kwa kuwasaidia wanyonge katika kuwasaidia Wakulima wa Zao la Korosho huku akisema ni Viongozi wachache waliofikisha Taifa katika hali mbaya hapo Rais Magufuli ameshaanza kurejesha heshima ya Taifa hili kwa kukemea mambo ya hovyo ikiwamo Ufisadi na kuwajibika kwa watumishi wa Umma.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Adam Maro , amewataka boda boda wote waliohitimu Mafunzo wawe mabalozi wazuri kwa wenzao ambao wameshindwa kupata hayo Mafunzo. Pia amesema wajitahidi kutii Sheria bila shuruti na kutojihusisha na ubebaji wa magendo pamoja na majambazi.
" Elimu hiyo muitumie vizuri , tunatarajia nyinyi muwe wasimamizi wazuri wa Sheria pamoja na kufichua waharifu hivyo vyeti hivi msiviweke ndani hakikisheni mnatembea ili tuweze kuwabaini wakina nani hawajasoma na wakina nani sio watiifu wa Sheria" Amesema OCD Maro.
Amesema ili boda boda waweze kuwa walinzi kamili lazima walinde Sheria.
Pia amewataka wale ambao wanatabia ya kutopeleka Pesa kwa mabosi wao ni dhuruma na chanzo cha umasikini kama wanahitaji Maendeleo wanatakiwa kuwa waaminifu katika kazi zao.
Hata hivyo, Kamanda wa Wilaya wa Usalama bara barani ( D.T .O), Inspekta Stanley kyunga, amewataka boda boda kutoingiwa na tamaa ya kubeba watu usiku kwa gharama kubwa aidha kwa kutambua watu hao ni waharifu au la.
Amesema asilimia ya Boda boda ni walevi hivyo wanapolewa wanapata nguvu ya kujiamini kupitia kiasi bara barani hatimaye kusababisha ajari bara barani. Pia kuhusu Leseni, amewataka kushirikiana nae kwani leseni zimegawanyika katika madaraja hivyo wapo vishoka walishawaliza wengi kwa kuwapiga bei za juu.
Katika upande wa Afisa Habari wa UMBV, Ndugu Msisiri, amewataka wale wote waliohitimu Mafunzo ya udereva wazkngatie Sheria na wawe mfano kwa wenzao .
pia amewataka wale ambao wanahitaji kujiunga na chama Chao wafike Ofisini kwa kufuata utaratibu husika kutoka kwa kikundi ambacho MTU anataka kujiunga.
Post a Comment