RC MAKONDA: "KWA SPEED HII YA RAIS MAGUFULI TATIZO LA MAJI DAR ES SALAAM LITABAKI HISTORIA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo amefanya mazungumzo ofisini kwake na *Katibu Mkuu* Wizara Maji *Prof. Kitila Mkumbo* ambapo wamekubaliana *kumaliza tatizo la maji* jijini humo na kulifanya kuwa *Historia* kama *ilani* ya CCM inavyoeleza kuwa ifikapo Mwaka *2020* upatikanaji wa maji utafikia *95%* na 2025 Kufikia *100%.*
*RC Makonda* amesema tangu *serikali ya awamu ya tano* iingie madarakani imafanya *jitiada kubwa* za kupanua wigo wa *upatikanaji wa maji* na hata maeneo yaliyokuwa na *ukosefu wa maji* kwa sasa *maji yanapatikana kwa wingi* jambo ambalo ameipongeza serikali.
Aidha *RC Makonda* amemuomba *Prof.Mkumbo* kufanya jitiada za kufikisha huduma ya maji maeneo ya *Kigamboni, Temeke, Chanika, Changanyikeni,Mbuyuni,Mbezi juu, Madale, Wazo, Mivumoni, Bunju, Tegeta A, Goba,Salasala, Mabwepande,Kimara, Mbuyuni, Pugu, Gongo la Mboto, Mombasa, Kipawa, Ukonga, Kitunda, Majumba Sita na Baadhi ya maeneo ya Kinyerezi na Bonyokwa* ambayo yanakabiliwa na *uhaba wa Maji.*
Katika mazungumzo hayo *RC Makonda* pia amemuomba *Prof. Kitila Mkumbo* kutolea *ufafanuzi* suala la *wananchi waliochimbia visima* vya Maji ambalo limezua *taharuki* kwa wengi wao kutokana na *mkanganyiko* uliojitokeza ambapo kwa Dar es salaam kuna visima zaidi ya *3,000* vya wananchi.
Akitolea *ufafanuzi* jambo hilo *Prof. Mkumbo* amesema *sheria ya rasilimali za maji ya mwaka 2009* inaeleza kuwa Kama Mwananchi atachimba *kisima nyumbani* chenye urefu wa *Mita 15* kwaajili ya *matumizi ya nyumbani* hatopaswa kuomba *kibali wala kulipia*, lakini kwa waliochimba visima na kuweka miundombinu Kama *Pump na mitambo* watapaswa *kupewa vibali na kulipia ada* ya mwaka huku wale waliochimba visima kwaajili ya *biashara au umwagiliaji* wakitakiwa kupata kibali na *kulipia ada.*
Sanjari na hayo *Prof. Mkumbo* amempongeza *RC Makonda* kwa namna anavyofanya jitiada za kuhakikisha *Wananchi wote wa Dar es salaam wanapata maji safi na salama* Kama serikali yao ilivyowaahidi.
Post a Comment