DC Mjema awataka Wazazi kuzingatia Lishe Bora.
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewashauri Wazazi Wilayani Ilala kunyonyesha watoto wao ili wawe na lishe bora.
Mjema aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa kumkataba Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala katika kutekeleza afua za lishe Manispaa Ilala.
"Wazazi nawaomba pindi mnapojifungua wanyonyesheni watoto wenu maziwa mpaka mda ufike msiwakatishe ni halali yao kwa ajili ya afya bora ya mtoto"alisema Mjema.
Aidha pia amewataka wananchi wake kula mro kamili na vyakula vya zamani kuachana na vyakula vya kisasa.
Alisema katika nchi yetu Tanzania inaitajika Taifa bora lipatikane kwa kuwa na afya bora aliagiza elimu itolewe shuleni,katika nyumba za ibada ili kukabiliana na utapiamlo.
Aidha amewataka wajumbe wa Kamati ya Lishe ndani ya Halmashauri ya Ilala kusimamia na kuakikisha wanapambana na changamoto za lishe duni .
Amewashauri wazazi kuakikisha wanawapa watoto wao haki za msingi katika lishe kina mama wanatakiwa wanawapa watoto wao virutubisho vizuri.
Alisema halmashauri ndio kitovu cha utekelezaji hapa nchini na ili kuweza kukabiliana na utapiamlo inatakiwa tuwe na mikakati na mipango thabiti kwa kutoa rasilimali fedha na watu na kila mdau kuonyesha bayana mchango wake katika kukabiliana na utapia mlo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri amesema upungufu wa lishe mwilini unaweza kuleta madhara mbalimbali amewataka wananchi wa ilala kura mro kamili kwa afya bora.
Aidha, DC Mjema, amesema Wanawake wengi wanajifungua kwa Operesheni kutokana ukosefu wa lishe kitu kinachowafanya kupelekea kukomaa kwa viungo vya uzazi
Post a Comment