Header Ads

Baraza la Madiwani Ilala laitolea uvivu TARURA kutokushirikishwa katika miradi ya Bara bara





.



Mstaiki Meya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko(Kushoto), Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne SHAURI(katikati), Pamoja na Katibu tawala wa Manispaa hiyo Sheila Edward (kulia).














Baadhi ya madiwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

























Naibu Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza Katika kikao Cha Madiwani Leo.




















Mwanasheria Mkuu we Wakala wa Bara bara TARURA Manispaa ya Ilala















BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,wamelalamikia Wakala wa Barabara TARURA Katika Manispaa hiyo kwa kushindwa kuwashirikisha Katika ujenziU ama Ukarabati wa Barabara katija kata.


Madiwani wa Ilala wametoa malalamiko hayo leo katika kikao cha baraza la nadiwani ambapo Diwani wa kata ya Upanga Mashariki Sultan Salim aliwasilisha malalamiko yake na kusema kuwa katika barabara za Mtaa wa Ismani Makao Makuu Jeshi na Urambo hazijakarabatiwa mpaka Sasa Jambo ambalo limekuwa Kero kwa wananchi.


" Sisi kama madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Ilala tunawataka TARURA watushirikishe wanapokuwa kujenga barabara katika kata zetu Kwani wananchi wanatupa lawama kutokana na utendajii katika barabara za wananchi wetu mfano katika eneo la makao makuu ya Jeshi utekelezaji unasua sua "amesema Sultan.


Amesema toka serikali kuikabidhi TARURA shughuli za barabara utekelezaji wake ndani ya manispaa ya Ilala umekuwa haufanyiki kwa wakati na hata Barabara nyingine kutojengwa kabisa.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara TARURA Mhandisi Samwel  Ndoven amesema Manispaa ya Ilala wametenga shilingi bilioni 6.2 katika bajeti ya mwaka 2018 hadi 2019 kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara .


Aidha Amesema ipo changamoto ya uhaba wa fedha zulizotengwa Jambo linalopelea kuwepo kwa Barabara nyingine zisizokarabatiwa.














Amesema wameanzisha mfumo ambao utaweza kuonyesha idadi ya barabara na gharama zake na kwamba mfumo huo umeshaanza kazi hivi karibuni Jambo litakalosaidiaa kugundua ni gharama kiasi gani kitumike Pamoja na Barabara zipi Bado.


Amesema Miradi ya Barabara itakayosimamiwa ya kuchonga barabara mbalimbali km 70 ambapo alitaja barabara zilizopo katika mpango huo ni Kitunda,Mwanagati,Kwampalange ,Tabata,Mawenzi,Kisiwani,Chanika,Msumbiji,Nzasa.

Barabara nyingine ni Kibeberu,Magore ,Kisukuru Makoka,Pugu Majohe ,Mondole,Kitunda ,Kipera,Bonyokwa ,Kisukuru,Kimanga Tasaf,Kivule ,Kinyerezi na Zimbili.








No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.