Header Ads

Mkurugenzi Ilala awatwisha zigo Madiwani kutoa Elimu ya lishe kwa Wananchi




MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri , amewataka Madiwani kushirikiana kutoa elimu ya lishe kwa Wananchi kupitia vikao vyao.


 Akizungumza hayo kwenye Ukumbi wa Anautogro Leo mapema kwenye uzinduzi wa Mafunzo ya kupanga mipango na Bajeti ya lishe Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa kama Madiwani hao wakiwa mstari wa mbele watawafikia watu wangi kupata uelewa juu  ya elimu ya lishe. Amesema Jamii nyingi hawana ufahamu kuhusu lishe hivyo Madiwani wanapokutana wanapaswa kutoa elimu hiyo kwa upana zaidi.


Pia amewataka wataalamu kufika Shuleni ili Watoto hao wapate taaluma hiyo mapema katika kupata kizazi chenye uelewa mkubwa na kuondokana na utapiamlo na udumavu.

" Tuna kila sababu ya kuelimishana elimu hii pana, ombi langu kwa Madiwani ninawaomba huko Katika vikao vyenu mtoe elimu hii kwa wananchi " Amesema Mkurugenzi Shauri.

Naye Katibu Tawala wa Ilala, Sheila Edward, amesema ili wafanikiwe katika Lishe lazima wajitangaze kupitia vyombo vya Habari .

 Pia amesema suala la  Lishe liwe ajenda kuu katika Mabaraza ya Manispaa na kata ili kupeana majukumu na kila mmoja aonyeshe jitihada za kupambana.

Kwa upande wa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto , amemshukuru Mkurugenzi Shauri kwa kauli yake na kumuahidi ushirikiano huku akisema  Bajeti ya Shilingi 1000 kwa Watoto Laki Moja na Elfu tisini na mbili  waliopo chini ya umri wa miaka 5 isibadilike.

Hata hivyo hakwenda mbali na kauli ya Mkurugenzi Shauri ya Madiwani kutoa elimu lakini aliomba kama upo uwezekano wa kurudishwa kwa Pesa za vikao kwa Madiwani litakuwa jambo zuri  kwani Pesa hiyo ilishafutwa.

Amesema kuwa Madiwani wanapenda kufanya vikao na Wananchi wao tatizo Bajeti hivyo watajitahidi kutoa elimu hiyo kadri inavyowezekana.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.