ARUMERU YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAANZA KUONEKANA
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru *Mhe. Jery Muro* amejitolea kuwasadia kuandika Maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze *KUKOPESHEKA* na taasisi za Kifedha ambazo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo au Andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.
Mhe Muro amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo Kwa *VIKWAZO* vya maandiko ya Mradi katika hatua za awali Pinda *wananchi* wenye nia ya kuanzisha kilimo na ufugaji wa kibiashara wanapoanza safari ya kutimiza *ndoto* zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa *vikwazo* hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia *wananchi* kuondoa Vikwazo hivyo.
Mhe Muro amesema *tayari* kampuni Binafsi ya Wawezeshaji wa wakulima *( PASS)* Private Agricultural Sector Support imekubalKuwaandalia na kugharamikia Mpango Kazi wa kibiashara *( Bussiness Planning )* zitakazowasaidia Wakulima na Wafugaji katika kupata Mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa Kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara.
Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Mhe Muro kufunga *MAONYESHO YA JUKWAA LA WAKULIMA MERU* ambayo yamefanyika Kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo pamoja na kukubali kutoa msaada wa BURE katika kuandaa na kuandika maandiko ya mchanganuo wa kibiashara pia amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji *JUKWAA LA WAKULIMA MERU* ili kuwawezesha kufanya kazi zao Kwa Haraka zaidi, na kuhaidi kuwatafutia Computer Kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu Za taarifa za wakulima na wafugaji.
Kwa upande Meneja wa Tawi la kampuni ya *( PASS)* amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru MHE Jerry Muro Kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi hao Kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na Taasisi hiyo.
Post a Comment