Mkurugenzi Ilala ataja vipaumbele kuinua uchumi wa Manispaa.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala , Jumanne Shauri, amesema vipo vipaumbele ambavyo wamevipa nguvu katika kuinua uchumi wa Manispaa na watu wake.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kukamilika kwa mkutano mfupi wa mjumuisho ya DC Mjema kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ,amesema Manispaa ya Ilala itaendelea kutumia rasilimali zilizopo ili kuleta maendeleo.
DC.
Amesema maendeleo ya kweli yanaletwa na mikakati yenye ushirikishwaji imara wa rasilimali pamoja na kubuni vyanzo vya mapato kama ilivyo ainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano , John Magufuli ya ukusanyaji wa kodi.
Aidha katika kuona hilo linakamilika na maendeleo yanapatikana, ametaja vipaumbele 10 vitakavyotumika katika kufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi ya Shilingi Bilioni 56 kwa mwaka tofauti na Manispaa nyingine hapa nchini. Vipaumbele hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo-:
1: Suala la kuboresha na kuongeza mapato Halmashauri yenye malengo ya kufikia Bilioni 56 kwa mwaka ambapo malengo hayo yatafikiwa baada ya kuboresha masoko , mfano Soko la Kisutu limetengewa Shilingi Bilioni 13.4 huku wakitarajia kukusanya Shilingi Bilioni 3 kwa mwaka.
Machinjio ya kisasa ya Vingunguti Bilioni 3 zimetengwa , mkakati wa kuwasaidia Wamachinga kwa kushirikiana na TRA , mpango wa kupanua vyanzo vipya mfano Stendi ya mabasi Chanika ambapo Milioni 160 zimetengwa kulipa fidia ili kupisha ujenzi na litakapokamilika watakusanya Milioni 600 kwa mwaka stendi hiyo ikikamilika huku mwezi uliopita walikusanya Bilioni 1.6 walikusanya.
2: Kuboresha na kuimarisha Mazingira elimu ya awali, Shule za Msingi na Sekondari, amesema dhamira yao ni kujenga Vyumba 500 vya madarasa.
3: Kuboresha huduma za Afya ya Msingi mfano kujenga Hospitali kubwa Kivule huku Milioni 500 Rais amewaingizia Manispaa na wao wametenga Milioni 250.
4: Fedha za ununuzi wa Dawa ili mwananchi asipate usumbufu wa kununua Dawa, amesema Milioni 500 Manispaa itatenga ili kupanua vituo vya Afya kulipa fidia watu waliopembezoni Mwa miradi.
5: Kuboresha huduma za upatikanaji Maji safi na Salama ambapo Manispaa imetenga Milioni 600 Maji yapatikane.
6: Kuimarisha miundombinu ya Bara bara na Madaraja ambapo Bilioni 600 zimetengwa katika mkoa wa Dar pamoja na kushirikiana na Benki ya Dunia. 7: Kuboresha na kuimarisha utii wa Sheria na utawala bora 8: Kuboresha huduma za Usafishaji na Mazingira ambapo Manispaa hiyo inategemewa na watu wengi katika uwekaji wa dampo la Taka taka.
9: Kuboresha huduma za umiliki wa ardhi, amesema Watendaji wanatakiwa kuwa makini wakati wa urasimishaji wa ardhi ili kuepuka migogoro baina ya Watendaji na wananchi.
10: Kuimarisha huduma za uwezeshaji kijamiikijamii mfano kuwakopesha Vijana Boda boda na mikopo ya 10% ya Vijana, Wakina mama na Walemavu.
katika hatua nyingine , Mkurugenzi amesema kwa Sasa wanajikita katika ukamilishaji wa vipolo vya miradi.
" miradi yote ya zamani tunataka kuhakikisha inakamilika ili twende katika miradi mipya" Amesema Mkurugenzi Shauri.
Post a Comment