Header Ads

Das Ilala awafunda wakina mama uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji kiuchumi Wilaya ya Ilala

.




















KATIBU Tawala wa Wilaya ya ilala  , Sheila Edward Lukuba, amewataka wakina mama kuacha maisha tegemezi Mara baada ya ufunguzi wa jukwaa hilo kuzinduliwa rasmi leo kwenye Kiwanja cha Mmnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

 Hayo ameyasema Leo wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la  Wanawake Ilala akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo, amesema Jukwaa limezinduliwa hivyo ni fursa kwa wakina mama kuacha maisha tegemezi kwani wao ndio wazalishaji wa kubwa katika familia. 

Amesema kuzinduliwa kwa Jukwaa hilo kutawezesha  kupatikana kwa mikopo ya uwezeshaji kiuchumi hivyo matarajio yake ni kuona Wakina mama wanatoka hatua moja kwenda nyingine kimaendeleo. 

 Amesema Makamu wa Rais wa Tanzania, Mh: Samia Suluhu, ameona mbali kwa kuja na wazo la  kuwawezesha wakina mama ili wawe Nguzo imara katika kuelekea Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.

 Amesema licha ya Mama Samia  lakini pongezi kubwa ziende kwa DC MJEMA kwa kuwakutanisha wakina mama wote na hatimaye Jukwaa limezinduliwa akiwa kama mlezi wa Jukwaa Mkoa wa Dar es Salaam.

 " Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kufanikisha uzinduzi wa Jukwaa hili, pia mama yetu MJEMA anawapenda sana amesema yupo pamoja na nyinyi hakuweza kufika kwa ajili ya changamoto lakini rai yangu uzinduzi huu uwe na faida sisi ndio wazalishaji katika familia usikubali kila kitu mwanaume pambana ili kutengeneza familia bora kwani Mwanamke anaweza ukiangalia Makamu wa Rais Mwanamke,  DC ilala ni Mwanamke, DC Kigamboni Mwanamke na katibu Tawala wote Kigamboni na Ilala Wanawake hii tafsri yake Rais ametuamini na sisi tujiamini" Amesema DAS.

 Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la  Mwanamke Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia alikuwa mgeni rasmi uzinduzi huo, Mariam Mungula, amesema huu si wakati wa kulala, Jukwaa tayari kanzi inaanza kuelekea uchumi wa Viwanda. 

Amesema  wakina mama walianza kuwezeshwa kufanya maonyesho na kupatiwa Elimu ya ujasiriamali hivyo anaamini kwamba wakati wa mabadiliko kwa Wakina mama ni huu. 

Amemshukuru Uongozi wa KCB Benki kwa kufadhili shughuli hiyo ya jukwaa pamoja na TCCIA kwa kuwa karibu nao na kushirikiana katika kutimiza miaka 30 ya kuanzishwa kwao hapa Tanzania.

 Amesema uwepo wa Benki hiyo utasaidia  kuwawezesha wakina mama kupata mikopo kwa Vikundi vyao ili vipige hatua.

 Amesema kama ushirikiano huo utaendelea kati ya Jukwaa na KCB Benki , basi moja kwa moja benki hiyo itakuwa imeunga mkono Juhudi za Mh Rais Magufuli  katika adhima ya kufika katika Tanzania ya Viwanda.



 " Serikali imeanza jitihada za kuwawezesha Wakina mama kwa kuwatengenezea mazingira rafiki katika kujikwamua na umasikini na maisha tegemezi" Amesema Mungula. Amesema kuwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya TCCIA unalenga kwa dhati ya kumkwamua Mwanamke kiuchumi. 

Amesema mpaka Sasa wanajumla ya Wanachama Elfu 27  katika Mkoa wa Dar es salaam na wapo katika kuhakikisha wanaongeza idadi hiyo kwa kumfikia kila Mwanamke katika mkoa wa Dar.   

 Kwa upande wake,  Mkuu wa Kitengo wa Biashara ndogo ndogo na kati KCB Benki , Masika Mukule, amesema wao wamejikita katika kuwasaidia Wakina mama na Vijana kwani wameanzisha programu za  kuwafundisha wafanya Biashara  jinsi ya kutunza Pesa na elimu ya mikopo pamoja na ujasiriamali. 

Amesema kwa nchi ya Tanzania Kilimo na Biashara ni uti wa mgongo wa uchumi. 

" Tumeanza kazi muda hapa Tanzania, lakini tumekuwa wachangiaji wakubwa wa pato la Taifa, mpaka tuna Matawi 220, ATM 1000 pamoja na Mawakala 1997" Amesema Mukule. 

 Hata hivyo, Kaimu Rais wa TCCIA, Ndugu Oktavian Mshpu, amesema watashirikiana na Jukwaa  kwa kuwawezesha kiuchumi kwani tayari wana Matawi ya Vijana  ( Youth Tccia Chember ) na Wakina mama ( Women chamber). 

Amesema kuwa miaka 30  Chamber  TCCIA wameweza kuongeza ushiriki  wa Watanzania katika Biashara. 

Amesema kipindi cha nyuma muamko wa uchumi kwa watu ulikuwa Mdogo sana tofauti na Sasa kwani 30% ya chamber kwa wakina mama ni ishara ya uchumi kwa wakina mama umepanda. " Tupo kwenye mkakati wa kufanya majadiliano katika kujenga uchumi pamoja na mikutano ya kibiashara ya kutafuta wawekezaji nchi za nje" Amesema Oktavian . 

katika hatua nyingine, Das Ilala, Sheila Edward Lukuba, amelitaka jukwaa hilo kuwa na mipango thabiti itakayo wafanya waweze kunyanyuka kiuchumi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.