Mratibu wa Umoja wa Ilala awawezesha Polisi Jamii Tabata
POLISI Jamii Tabata Mtambani wapokea msaada wa reflectar kwa ajili ya walinzi vilivyotolewa na Mratibu wa Ilala Heri Shaaban ..
Akizungumza wakati wa kukakibidhi msaada huo Heri Shaaban alisema suala la ulinzi ni letu sote kila mtu ana wajibu wa kulinda na kusaidia Polisi Jamii.
Shaaban alisema yeye ni mlezi wa Sungusungu wa Tabata Mtambani awali kabla kukabidhi msaada huo aliwakabidhi virungu kwa ajii ya kutumika katika lindo..
"Awali nilikabidhi virungu ili wavitumie katika lindo nyakati za usiku kwani wanakutana na changamoto nyingi katika lindo ikiwemo vitendea kazi ,wakati nawapa virungu waliomba niwatafutie sare ili usiku waweze kutambulika kwa urahisi ambapo leo nimetekeleza kwa kugawa Reflectar"alisema Shaaban
Shaaban alisema kila sungusungu ambaye atakuwa Tabata Mtambani atavaa hiyo Reflectar itakuwa na maandishi ya kuwatambulisha Polisi Jamii Tabata Mtambani mda wote wanalinda mchana na usiku na uwepo wao kwa sasa imesaidia uhalifu kupungua katika mtaa huo wananchi wanaishi kwa amani.
Shaban aliwataka wananchi wa Mtaa huo kulipa ada ya ulinzi kwa wakati ili ziweze kutumika katika uwendeshaji wa ofisi yao na kununulia vitendea kazi.
Aidha pia aliwataka Polisi Jamii wawe wamoja wasiweke mpasuko na viongozi wao.
Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Salum Hamduni anatarajia kuzindua rasmi Polisi Jamii Tabata Mtambani hivi karibuni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tabata Mtambani Brigita Nchimbi alipongeza kupokea msaada huo katika Mtaa wake kwa sasa uhalifu umepungua Jeshi la Mtaa huo linafanya kazi nzuri wanashirikiana na Polisi wa Kituo kikuu cha Tabata.
Naye Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Tabata Mtambani Mjata Hiza alisema Ulinzi Shirikishi ni wetu sote ni moja ya jukumu lake katika Mtaa kuangalia usalama wa Mtaa wake .
Mjata alisema katika Mtaa wa Tabata Mtambani ana mikakati ya kuongeza askari wa kulinda na kuboresha mazingira yao ya kazi.
Post a Comment