DC Mjema afungua Semina ya uendeshaji wa mifuko ya kuendeleza Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, Leo amezindua rasmi Semina ya Uendeshaji wa Mfuko wa Kuendeleza Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Semina hiyo inayolenga kutoa mikopo Katika Manispaa ya Ilala , imehusisha Madiwani, Watendaji, pamoja na Wakuu wa Idara ambao ndio watu wa kwanza katika utoaji wa Elimu ya mikopo kwa Wananchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo kwenye ukumbi wa Anautogro, DC Mjema, amesema kuwa semina hiyo iwe na manufaa na majukumu yaliyobainishwa katika Mafunzo hayo wahakikishe yanafanyiwa kazi.
Aidha amesema kuwa Mafunzo yaliyotolewa leo yawafikie Wananchi ns kuhakikisha wanakuwa na nidhamu.
Amesema kuwa kupitia Mafunzo hayo ipo haja kuweka mikakati madhubuti ili mikopo hiyo iwafikie Wananchi kwa haraka.
"Tunaenda katika utoaji mikopo, kuna haja ya kila mmoja wetu kutoa elimu kwa Wananchi wake, hivyo hii mikopo isitolewe kiholela lazima muangalie watu hao wamekidhi vigezo maana ili watu wapate hiyo mikopo katika maombi yao lazima Vikundi hivyo viwe vina shughuli za kufanya" Amesema DC Mjema.
Amewataka Wananchi wanaokopa Pesa hizo wasipitilize muda wa marejzisi ili kuweza kuwapatia na wengine lakini kitendo cha kuchelewa kurudisha Pesa kosa la jinai linaloweza kupelekea mkopeshwaji kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema wale wanaokopa wasitumie Pesa hizo kwa ajili ya starehe bali watumie mikopo hiyo katika kuendesha Biashara zao na kurudisha mikopo hiyo kwa wakati.
Amewataka wahusika wahakikishe Pesa hizo za mikopo zisimamiwe vyema katika utaratibu mzuri ili kuweza kutimiza mipango iliyokusudiwa.
DC Mjema, amesema hadi kufikia mwakani Novemba anataka kuona Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inaongoza kwa kuwa na bidhaa bora kuliko Manispaa yoyote hapa nchini.
Amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, kuhakikisha anashirikiana vema na Taasisi kama vile T.R.A, T.B.S ili iwe rahisi kwa wananchi kufahamu wapi wanaweza kupata misaada ya kuendesha mikopo.
" Hii Mkurugenzi ukiifanya kwaHizo Taasisi itasaidia wafanya Biashara kwenda katika Taasisi hizo ili kuboresha bidhaa zao maana sio wote wanajua umuhimu wa TBS na TRA lakini mkiwaunganisha huko hata mapato yetu tutakusanya kirahisi na kuongeza ubora wa bidhaa Katika Manispaa yetu"Ameongeza DC Mjema.
Katika kuona semina hiyo ya Mafunzo inakuwa na tija basi kila mjumbe ahakikishe baada ya kutoka hapo basi aende kutatua kero za Wananchi.
Hata hivyo amesema ipo haja ya wafanya Biashara hao baada ya kupewa mikopo wafuatiliwe kwa umakini ili Vikundi hivyo viweze kupeleka bidhaa zao Supermarket na hata nchi za nje.
Mbali na mikopo amesema kuwa lazima Wananchi hao wawe na Afya nzuri kwa kuzingatia kupata lishe bora kwani nchi za nje zimeendelea kutokana na kupata lishe yenye virutubisho na kuwafanya kuwa na idadi kubwa ya Wanasayansi wengi.
Katika kuona mikopo hiyo ina kwenda kuwa suluhisho la matatizo lazima Viongozi watatue kero za Wananchi kwa kutembea mtaa kwa mtaa kama Kata ya Upanga Mashariki walivyoanza.
Hivyo ametoa rai kwa Madiwani ambao hawajaanza zoezi hilo waanze Mara moja ili kutatua kero hizo.
Semina hiyo ya Mafunzo ya mikopo ni moja ya agizo la Halmashauri zote nchini kutenga na kupeleka asilimia 10% ya mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani kwenye mfuko wa kuendeleza Wanawake na Vijana.
Naye Meya wa Manispaa ya ilala, Charles Kuyeko, ameupongeza Uongozi wa Manispaa ya Ilala kwa kupata hati safi. Amesema mikopo itakayotolewa kwa Wananchi irudi ili iwafikie wengine.
Post a Comment