DC KATAMBI AFICHUA FURSA SITA ZA KIBIASHARA DODOMA
UKIWA zimebaki siku tano kufanyika kwa kampeni ya Fursa sambamba na Tamasha kubww la Fiesta jijini Dodoma, Mkuu wa Wilaya hiyo, Patrobas Katambi amefichua fursa sita zinazopatikana ndani ya Wilaya hiyo.
Katika mahojiano maalum na Kituo cha Radio cha Clouds FM na Clouds TV, DC Katambi ametaja fursa hizo kuwa ni pamoja na Kilimo, Biashara, Ardhi, Hoteli, Ujenzi na Vitega uchumi mbalimbali.
Amesema fursa zilizopo ni nyingi ikiwemo Kilimo nq Biashara ambapo amesema Kilimo cha umwagiliaji kinawezekana huku akitaja mazao yanayolimwa Dodoma kuwa ni Zabibu, Pamba, Alizeti na Mtama.
“ Zipo fursa kubwa ambazo pia zimechangia Dodoma kuwa Jiji ni uwepo wa shughuli mbalimbali za ujenzi wa miradi mbalimbali mikubwa zinazoendelea, maeneo yanatwaliwa lakini wananchi wanalipwa fidia, katika hizi fidia wanazolipwa kwao ni fursa maana zinawawezesha wao kiuchumi.
“ Vilevile kuna fursa za uwekezaji mfano mahoteli, kama Mji Mkuu na Makao Makuu ya Nchi tunahitaji sana Hoteli za kisasa za Nyota tano na nyota tatu, tunahitaji kuwa na supermarket kubwa, shopping malls za kutosha maana watu wote wanakuja Makao makuu ya Nchi hivyo tutoe rai kwa wafanyabiashara kuja kuwekeza,” Amesema Katambi.
Amesema eneo lingine ambalo ni fursa ni ardhi ambapo wanauza kwa taasisi na watu binafsi kwa maana ya kuweka makazi, Biashara na maeneo ya viwanda ambapo lengo lao ni kuhakikisha wanalipanga jiji ili kuwa katika mpangilio wa kisasa.
Post a Comment