Zahera akerwa na ushindi kiduchu
KOCHA WA YANGA, MWINYI ZAHERA PICHA NA MTANDAO
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa anachukia kuona timu yake inapata ushindi "mwembamba" na kuwaagiza washambuliaji wake wabadilike katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zinazofuata.
Ushindi mkubwa ambao Yanga wameupata msimu huu ni wa mabao 3-0 dhidi ya Alliance FC kutoka Mwanza walipowakaribisha kwenye Uwanja wa Taifa.
Zahera alisema kuwa sasa anataka kuona washambuliaji wake wanatumia vizuri nafasi wanazozipata ili waweze kufunga idadi kubwa ya mabao ambayo anaamini yatawasaidia katika hatua za lala salama za ligi hiyo.
“Lazima sasa tubadilike na tupambane, nataka kuona tunatumia vyema nafasi tunazozipata katika michezo yetu, tunakuwa na uwezo wa kupata ushindi mkubwa zaidi lakini tunakosa umakini kwenye umaliziaji, nataka hilo liondoke kwetu,” alisema Zahera.
Aliongeza kuwa, anataka kuona mabadiliko yanaonekana kuanzia mchezo wa kesho watakapoikaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa.
Alisema anafurahi kuona wachezaji wake waliokuwa majeruhi wamerejea kwenye mazoezi akiwamo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu baada ya kupona majeraha yake pamoja na beki Andrew Vincent ‘Dante’.
Wakati Zahera akiwataka washambuliaji wake kupachika mabao ya kutosha kuanzia kesho, mahasimu wao, Simba wamekuwa timu pekee iliyovuna mabao mengi mpaka sasa ikiwa imecheza mechi 10.
Katika michezo miwili ya mwisho, Simba imevuna jumla ya mabao 10 huku ikiruhusu goli moja kwenye ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Alliance FC na 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlanzidi, Pwani.

Post a Comment