Header Ads

DAS ilala aungana na SEDIT kuadhimisha wiki ya Vikoba kwa kufanya usafi.









KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ilala, Sheila Edward Lukuba, Leo ameungana na Shirika lisilo la  Kiserikali linalojihusisha na VIKOBA hapa nchini katika kusherekea maadhimisho ya wiki ya VIKOBA Tanzania kwa kufanya usafi wa kusafisa bara bara katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.

 Katika maadhimisho hayo , miongoni mwa  Viongozi waliohudhuria ni pamoja na Diwani wa kata ya Ilala , Ndugu Saady Khimji, Afisa Mtendaji wa Kata, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amana pamoja na Watendaji wa kata hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kumalizika kwa zoezi la  usafi, DAS ameupongeza Uongozi mzima wa Shirika la  SEDIT VIKOBA kwa kuwa wabunifu Katika kujali swala la  usafi na Mazingira kwenye maeneo yenye mkusanyiko katika kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya Tano kuhamasisha Kampeni ya usafi.

DAS amesema Vikoba ni mfumo wa kuweka na kukopa kwa Wanachama waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

Amesema mfumo huo ulianza miaka 10 iliyopita na umekuwa na mafanikio makubwa kwa Wanachama kukopeshana na kusaidiana katika matatizo mbali mbali ikiwamo kuanzisha miradi ya kiuchumi.

 Pia amesema VIKOBA husaidia kutoa Mafunzo ya kuongeza ujuzi wa Biashara kwa Wanachama.

Amesema Mafunzo hayo yanaongeza ubora wa vitu vinavyozalishwa ili kupelekea ongezeko la  faida kwenye Biashara.

Amesema kwenye VIKOBA hutoa fursa kwa kutengeneza bidhaa mbali mbali ikiwamo sabuni za Maji pamoja na namna bora ya kufungasha.

 Amewataka watu waendelee kuamini mfumo wa VIKOBA kwa husaidia kutafuta masoko ya uhakika ya kusambaza na kuwa na bidhaa kwa bei  yenye faida.

Amesema kimbilio la  wengi  liwe kwenye kuwekeza nguvu katika VIKOBA kwani ndio njia ya kupatia mitaji ya Biashara ya kuanzisha au kuendeleza Biashara hivyo hupelekea kutoka kwenye hatua ya mtaji Mdogo kwenda mtaji mkubwa.

Licha ya kuelezea faida hizo, amesema yote hayo yatafanikiwa kama nidhamu , utii wa Sheria za nchi, ulipaji kodi, ubunifu pamoja na ushirikiano.

 Amesema wote waliopo katika VIKOBA ni matajiri wa baadae kama wakina Mengi, Bakhresa kwakuwa Serikali ya awamu ya tano ipo  bega kwa bega  katika kuwanyanyua wananchi wenye kipato cha chini ili wafike kwenye uchumi wa kati katika kuelekea Serikali ya Viwanda.

 " Serikali yetu imejidhatiti kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na rasilimali zilizopo kwani katika awamu hii ya Rais John Magufuli imeona  haja ya kuwajali wanyonge na masikini kwa kutoa mikopo bila riba, Manispaa tuna mikopo yenye 10% kwa Vijana, Wakina Mama pamoja na walemavu hivyo hii ni fursa tunaomba mchangamkie" Amesema DAS. .

Pia amewataka Wakina mama kujitahidi kujiunga na  Jukwaa la kumuwezesha  Wanawake kwani mlezi wa Jukwaa hilo Katika Mkoa wa Dar ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh: Sophia Mjema hii ni Bahati pekee kwa Wana Ilala.

 Amewataka Wanawake kuchangamkia fursa kwani Wakina katika umoja huo wa VIKOBA utapunguza kushinda vibarazani  na kusaidiana Katika sherehe, Msiba , kuugua, pamoja na shughuli mbali mbali.

  Naye Diwani wa Kata ya Ilala, Mh: Saady Khimji, amesema kila Shirika la  VIKOBA wawe ns utaratibu wa usafi katika kuimarisha ubora wa Afya za wananchi.

Amesema SEDIT wameonesha kitu kikubwa kwa kuwa karibu na huduma za kijamii hivyo wazidi kuwa na moyo huo huo kwani pasipo na Afya hata maendeleo yake huwa na shida.

" Nimeona Juhudi za ndugu zetu wa SEDIT tuna kila sababu ya kuwashukuru kwa Upendo wao kuonesha wanajari Mazingira na usafi hii ni kampeni tosha ambayo inatakiwa kufanywa na Mashirika mengine" Amesema Khimji.

 Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa SEDIT VIKOBA , Bibi  Zainabu Orty, amemshukuru Katibu Tawala kujumuika pamoja  na ni faraja kubwa kuona Serikali inaunga mkono Juhudi zao . " Tunafuraha kubwa kuwa na Uongozi wa Wilaya, sisi tumeamua kufanya usafi katika Hospitali hii kutokana ns ukaribu tulionao pamoja na Kata husika tunayoishi, lakini maadhimisho mengine tutajipanga tofauti " Amesema Bibi Zainabu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.