Header Ads

MCT yavitaka vyombo husika kuchunguza kupigwa na kutekwa kwa waandishi.






Baraza la Habari Tanzania(MCT) limevitaka vyombo husika kuyafanyia uchunguzi matukio ya waandishi kupigwa kutekwa na kunyanyaswa na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya utoaji haki.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Kajubi Mukajanga ameyasema hayo wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukatili na jinai dhidi ya wanahabari ambapo amesema baraza hilo linatoa wito kwa vyombo vya usalama kukumbuka kuwa wanahabari ni kama raia wengine wana haki ya kulindwa wao na vitendakazi vyao.

Aidha Bw Mukajanga amesema kuanzia mwezi January hadi mwezi Oktoba mwaka huu jumla ya waandishi wa habari 35 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wamekumbwa na mikasa mbalimbali wakati wakitimiza majukumu yao.

Mukajanga amesema kwa mujibu wa kanzi data ya MCT waandishi hao wamekumbwa na mikasa ya kunyimwa taarifa, kutishwa, kutekwa, kukamatwa bila hatia, kutukanwa, kulipishwa faini, kuondolewa kwa nguvu katika eneo la tukio wanaloripotia, kuharibiwa vifaa vya kazi pamoja na kuhusishwa na makosa ya kimtandao.

Hata hivyo baraza hilo limewataka wana habari kuendelea kuripoti matukio yote ya ukiukwaji wa haki za waandishi yanayowakuta lakini pia kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.