Rais wa TBF aunguruma kuelekea Taifa Cup.
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu hapa nchini (TBF), Phrase Magesa, amesema sababu kubwa ya michuano hiyo kusogezwa mbele ni kutoka na kutoa nafasi kwa Mkoa wa Simoyu kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Kisasa ambapo fainali hizo zitafanyika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo kwenye Viwanja vya Gymkhana Jijini Dar es Salaam,amesema Mashindano hayo yatafanyika Desemba 15 hadi 20 ambapo jumla ya Mikoa 26 watashiriki.
Amesema uwepo wa Mashindano hayo yatapelekea kuweza kuchagua timu ya Taifa ya Wanaume na Wanawake. Licha ya kukamilika kwa baadhi ya maandalizi, amesema bado wanahitaji wafadhili ili kuweza kunogesha Mashindano hayo.
" Tunaelekea Mkoani Simiyu, tunaenda kufanya kazi kubwa itakayotoa matunda mazuri katika Timu zetu za Taifa , hivyo ni muhimu kila Mkoa kujiandaa vya kutosha kuleta ushindani" Amesema Magesa.
Pamoja na hayo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mh: Anthony Mtaka, kwa kazi nzuri ya kukuza mchezo wa Kikapu hapa nchini na kuwataka Wakuu wa Mikoa na Watendaji wote waige mfano wake.
Amesema wanatarajia kufanya Mkutano maalumu wa TBF kwa ajili ya kuboresha marekebisho ya Katibu yao ili kwenda mbele zaidi.
Vile vile ameongeza kuwa wapo katika mpango wa kuanzisha Ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 16 wakiwa na lengo la mwakani timu hiyo ishiriki michuano ya Kimataifa. Amesema timu za Wasichana kutoka Arusha na Wavulana kutoka Dar ambapo watatumia Uwanja wa Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park.
Hata hivyo amesema mwaka huu Desemba wanatarajia kupata wachezaji 12 wawakilishi kwenda Marekani na Canada.
Katika hatua nyingine amesema mwisho wa mwaka wanatarajia kuwa na zoezi la ugawaji tuzo kwa Wanamichezo bora pamoja na Waandishi walioripoti sana Habari zao katika kukuza Tasnia ya Mpira wa Kikapu hapa nchini.
Post a Comment