Header Ads

KIKAO CHA PAMOJA KAMATI YA MAENDELEO KATA ILALA NA MKUU WA KITUO CHA POLISI PANGANI








Leo Kata ya Ilala kulikuwa na kikao baina ya Kamati ya Maendeleo ya Kata na Mkuu wa Kituo cha Polisi Pangani Inspector Nyalala ambaye ameripoti hivi karibuni kuwa OCS wa Kituo hiko mara baada ya Afande Mama Swebe kupanda cheo kuwa OCD Wilaya ya Iringa Mjini.

Agenda kuu ya kikao hiko zilikuwa mbili:-

*1. Kutambuana*
*2. Mkakati wa Ulinzi na Usalama Kata ya Ilala.*

Kikao kiliendeshwa vyema kabisa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Ilala *Mhe Saady Khimji* Diwani wa *Kata ya Ilala.*

Mkuu wa Kituo alitoa taarifa mbalimbali ya kiusalama katika eneo letu la Ilala lakini kikubwa alisisitiza juu ya Ulinzi shirikishi katika Mitaa yote Mitano ya Kata ya Ilala.

Aidha alizungumzia juu ya kupokea taarifa maeneo yote yanayohusishwa na uhalifu lakini pia wauzaji wa Madawa ya Kulevya sambamba na Pombe haramu na Madangulo.

Alikiahidi kikao atashirikiana na Wenyeviti wa Mtaa kama wenyeviti wa Ulinzi na Usalama katika Mitaa kuhakikisha wanatokomeza uhalifu wa aina zote.

" Ilala kumekuwa na tabia za kiuhalifu ndani ya siku mbili tatu za hivi karibuni umefanyika uhalifu Mtaa wa Karume, wizi wa spear za Magari kwa wezi kutoboa ukuta lakini pia Mtaa wa Amana barabara ya Uhuru wezi wamevunja Duka la Used electronics na kuiba TV kubwa sita na vitu vinginevyo, hiki ni kiashiria kuwa wizi upo na wahusika kwa maana wezi hao wanapata ushirikiano na wenyeji wa maeneo hayo, niwaahidi viongozi tutaisafisha Ilala, biashara haramu zote tutazikomesha lakini pia madangulo, night club zisizo rasmi nazo zitashughulikiwa kikamilifu", alimalizia kusema Inspector Nyalala.

Baada ya Mipango na Mikakati kukamilika juu ya Ulinzi na Usalama Diwani wa Kata ya Ilala alimshukuru sana Insp. Nyalala kwa ujio wake lakini kwa ushauri na nasaha zake katika kuimarisha Ulinzi na Usalama Kata ya Ilala.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.