Header Ads

DC mjema asema Operesheni ya Majengo hatarishi haitamuacha mtu salama.



  

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, ameanza ziara ya kukagua Maghorofa hatarashi ambayo yapo kwenye hatari katika Wilaya yake.

Akizungumza na Waandishi wa  habari, DC Mjema, amesema hiyo ni  ziara yake  ya kwanza ya kukagua Maghorofa hayo baada ya kuahidi kurudi tena Novemba 30, 2018 kufuatia kumalizika kwa ziara zake za Majimbo kutatua kero.

 Amesema lengo la  ziara hiyo ni  kuweza kubaini Majengo yote ambayo hakuridhishwa na ujenzi wake ili kuzuia hatari kwa Wananchi ya kupoteza Maisha.

Amesema kuwa wapo baadhi ya wamiliki wakishirikian na wajenzi wanavuka utaratibu walioupata kutoka kwenye body ya majengo ya usanifu Wa ramani hivyo matokeo yake  ghorofa husogelea mwenzake au kutengeneza nyufa.

" Kuna baadhi ya wamiliki Wa mijengo sio waaminifu utakuta mtu  kibali chake kina mwambia ghorofa 10 yeye anazidisha 15 sasa hii in hatari watendaji na wahandisi hebu fuatilieni haya kwa haraka ili kuzuia hatari msimu Wa mvua unakuja upepp mkali ukivuma hatari itatokea kama ilivyotokea ghorofa la  akbaru" Amesema DC Mjema.

 Amesema operesheni hiyo ni endelevu hivyo kama mtu  atagundulika ghorofa yake  ujenzi hauna vigezo na haurizishi atabomolewa. Hata hivyo amesema ukaguzi huo utasaidia sana kuepusha hatari na huko mbeleni yasijirudie makosa ya ujenzi kama huo.

 Katika hatua nyingine, DC Mjema, amewataka watendaji kufuatilia Maghorofa ambayo hayajawekewa wavu wakati shughuli za ujenzi zinaendelea kwani kutoziba kunaleta hatari ya kudondoka kwa dhana na kumfikia mwananchi kumsababishia madhara au hata kifo.

Amewataka wale wanaokosa maeneo ya kujenga ghorofa na kujipenyeza waende hata  pembezoni Mwa Ilala kama vile Chanika maeneo yapo atawapatia.

" Nataka niwaambie  Hawa ndugu zangu hususani hawa waburushi sio lazima ghorofa ujenge mjini, najua wasi wasi  wenu ni ulonzi kwa vile maeneo yote ya Upanga na mjini yana ulinzi Wa kutosha lakini Chanika kule Mimi nitawapa maeneo ili mpanue Miji  Kamanda wetu Mambosasa amesema Dar yote ni salama hamieni huko kwanza Manispaa yangu tupo kwenye mpango Wa kujenga vituo vya polisi pembezoni pamoja na vituo vya ukusanyaji wa  Kodi iwe rahisi na kuepusha usumbufu Wa kuja Anautogro"Ameongeza DC Mjema.

Amesema zoezi hilo linatarajia kufanyika katika maeneo kama vile City Center,  Kariakoo, Upanga na Mtaa Wa Mindu ambapo zoezi hilo  limeanzia ambapo kufikia 30 Desemba,2018 zoezi hilo litakamilika na litatoa majibu ghorofa ngapi zimepigwa faini, ngapi zinabomolewa na ngapi zipo kwenye maboresho.

Naye Mhandisi Mkuu Wa Manispaa ya ilala, Eng. John Magori, amempongeza DC Mjema kwa ziara take hiyo huku akisema kasi hiyo itapunguza ujenzi holela usiofuata utaratibu.

Amesema kuwa halo hiyo inatokana na Wamiliki Wa Majengo hawahusishi wakandarasi hivyo kujikuta wanaingia katika hatari.

Pia amesema watahakikisha wanasimamia vyema utaratibu wa ujenzi ili kuzuia hatari kwa wananchi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.