*RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE"
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, leo amekabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania *JWTZ* na Jeshi la Magereza kwaajili ya kuongezea *ufanisi* katika utendaji wa Kazi wa *vyombo vya ulinzi na usalama.
Mabasi 4.aliyoyakabidhi , RC Makonda, Leo ni Kati ya Mabasi 11 yaliyokuwa yamekufa (ukweche) ambapo baada ya ,RC Makonda, kuyaona na kubaini uhaba wa magari kwa vyombo vya ulinzi na usalama aliwatafuta wafadhili wa Kampuni ya Dar Coach Ltd*waliojitolea kuyarejeshea uhai* magari hayo na hatimae leo yanatembea Barabarani yakiwa mazima.
*RC Makonda* amesema ukarabati wa mabasi hayo ulihusisha *Kubadilisha Bodi, kupaka Rangi, kubadili Viti, kuweka Mfumo wa kuchaji simu, AC, TV, Taa,Madirisha, Matairi* pamoja na kuongeza na kupunguza idadi ya viti.
Aidha *RC Makonda* amesema mkakati wa *kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama* utaendelea ikiwa ni pamoja na *kugusa maisha ya mtumishi mmojammoja* kwa kuwapatia mikopo ya viwanja vya bei nafuu.
Hata hivyo *RC Makonda* ameshukuru Kampuni ya *Dar Coach Tanzania Ltd* kwa uzalendo walioonyeaha kukarabati magari hayo *pasipo kutumia pesa ya serikali.*
Kwa upande wake *Mnadhimu Mkuu* wa Jeshi la Wananchi *Luteni Jenerali Yacoub Mohamed* amempongeza *RC Makonda* kwa ubunifu wa kufufua *magari yaliyokuwa yamekufa* ambapo ameeleza kuwa yatasaidia kwa kiasi kikubwa *kuwaongezea ufanisi katika kazi kwa kupunguza changamoto ya usafiri.*
*Mabasi 4* yaliyokabidhiwa leo ni *Ashok Leyland 01, Iveco 2 na Toyota Coaster moja* huku magari mengine *7* yakiwa hatua ya mwisho kukamilika.
Post a Comment