DC Mjema mgeni rasmi mahafali ya 36 Shule ya Chekechea Chesham Oysterbay.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema ,Leo amehudhuria kwenye mahafali ya 36 katika shule ya Chekechea Chesham iliyopo Oysterbay kwenye Viwanja vya St. Peter Jijini Dar es Salaam akimwakilisha Mke Wa Mh: Rais John Magufu, Mama Janeth Magufuli kwenye mahafali hayo.
Akizungumza na Waandishi Wa habari Leo, DC Mjema, ameupongeza Uongozi wa Shule hiyo kwa kuandaa mahafali hayo na kuwalea watoto katika maadili ya kiroho na yenye kumjua Mungu.
Amesema ni vizuri watoto wakajengewa misingi ya hofu ya Mungu ili kutengeneza Taifa lenye kulinda Amani na usalama wa wananchi.
Aidha amesema wapo Wazazi ambao wanawaua watoto kwa imani za kishirikina huku akisema Pesa zinapatikana kwa kufanya kazi na sivinginevyo.
Amewataka wazazi kuwasimamia watoto wao hususani katika mitandao ya kijamii ambapo inaweza kuwa na athari kubwa za Mtoto kuiga tamaduni mbaya kutoka huko. Amesema kuwa Viwango vya ukatili kwa watoto upo juu sana, hivyo ni jukumu la mzazi kuweka ulinzi pindi anapoona Mtoto yupo mbali na macho yake.
" Wazazi tuna jukumu kubwa la kuwalea watoto wetu sio kuwaachia waalimu peke tuhakikishe Mtoto anaporudi shule anajisomea na usimwache na mtu ambaye haeleweki lazima Mtoto awe karibu na kuzungukwa na watu sahihi katika familia"Amesema DC Mjema.
" Utakuta Mtoto anakuaga anakwenda kujisomea anarudi kesho na wewe mzazi unalizika kabisa lazima ujue alipokwenda na uhakikishe huyo mtu ni sahihi kwake,? Pia kuwalaza watoto na ndugu hili ni tatizo kubwa sana ukiangalia katika tafiti zetu watoto wengi waliobakwa, kulawitiwa husababishwa na mfumo huo, kuwa karibu na mwanao pia kwenye harusi huko tubadilishe kipengele kinachosema ,"Watoto tunawapenda lakini hawaruhusiwi, basi sisi tuseme watoto tunawapenda lakini wanaruhusiwa ili tuwe karibu na ulinzi " Ameongeza DC Mjema.
Amesema Wilaya ya Ilala takwimu zinaonesha kwamba watu 99 wamebakwa kutoka mwezi Julai hadi Septemba.
Amesema wakati Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa Viwanda lazima wazalishwe wataalamu wengi Wa Sayansi na wale wanajua lugha mbali mbali watasaidia kuwa wakali mani katika viwanda hivyo katika uwekezaji kutoka mataifa ya nje.
Naye Makamu Mwenyekiti Wa Shule ya Chekechea ya Chesham, Ndugu Joseph Silvester Kihwele, amempongeza DC Mjema kwa kuwa karibu nao huku akimtakia utendaji mwema katika Wilaya yake.
Amesema ni jukumu la wazazi kuhakikisha Mtoto ile tabia aliyotoka nayo shuleni hapo kuiendeleza hatimaye kufanya vizuri mbeleni.
Amesema wataendelea kutoa elimu nzuri kwa watoto katika shule yao hivyo amewakaribisha wanaotaka kujiunga shule hiyo fomu zipo.
Y
Hata hivyo katika hotuba yake DC Mjema, licha ya kutoa somo Akizungumza na Waandishi Wa habari Leo, DC Mjema, ameupongeza Uongozi wa
Post a Comment