Header Ads

MHE.ABOOD ATAJA MGAWANYO WA K.M 21.5 ZITAKAZOJENGWA KIWANGO CHA LAMI MANISPAA YA MOROGORO.


MBUNGE wa Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amesema kuwa Jimbo la Morogoro Mjini, limepokea Jumla  ya K.M 21.5 za Barabara zitakazojengwa kwa Kiwango cha Lami  Kupitia Mradi wa TACTIC yaani Mradi wa Uboreshaji Miji,

Mhe. Abood, amesema kuwa , Mradi huu umekwisha sainiwa na Serikali kuu ya Tanzania Kupitia O-R TAMISEMI na  BENKI YA DUNIA(WORLD BANK) ambapo Mradi huu utagharimu Fedha za Kitanzania karibuni Bilioni hamsini(Bil.50) hii ikienda sambamba na Ujenzi wa Standi ya Magari Eneo la station ya Reli ya Mwendokasi (SGR) Kihonda Mwaka wa Fedha 2022/2023.

Miongoni mwa mgawanyo huo wa  KM  ni pamoja na  K.m 17 Kata ya Tungi, KM 3.5 Kilimanjaro -Kihonda kutoka Reli ya Mwendokasi (SGR), na KM 1 ni kwenda Stesheni ya Reli ya Mwendokasi (SGR).

 Aidha, Mhe. Abood, amesema Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imepewa Jukumu la kutafuta Consultant(Mshauri Mtaalam wa Kiinjinia atakayehusika na Upembuzi Yakinifu wa Mradi) Kutangaza tenda na Kumpata Mkandarasi.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.