MAADHIMSIHO SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KATA YA MAFIGA YAFANA.
KATA ya Mafiga Manispaa ya Morogoro imedhimisha kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani pamoja na kuadhmisha Siku ya Lishe Duniani.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Juni 14/2022 kwenye Ofisi ya Kata ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku hiyo ambayo Manispaa ya Morogoro ifanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwembesongo Juni 16/2022.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi ambaye ni Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winferd Kipako, amewataka wazazi kuwajali na kuwapenda watoto wao kwani waliwaleta duniani kwa mapenzi yao wenyewe yawapasa kuwalea na kuwakinga na ukatili wa kijinisia.
Kipako, amesema kuwa, wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha masomo watoto hao.
"Hakuna mtoto aliyeomba kuja duniani bali ni sisi wazazi kwa starehe zetu tumewaleta hawa watoto na lazima tuwajali na kuwalinda, kuwapa elimu na pia kutowakatisha masomo yao na kupelekea ndoa za utotoni," Amesema Kipako.
Na kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, amesema kuwa watoto ni tuni ya taifa yapaswa kulindwa kwani kauli mbiu ya mwaka huu katika siku ya mtoto wa Afrika kwa hapa nchini inayosema TUIMARISHE ULINZI WA MTOTO; TOKOMEZA UKATILI DHIDI YAKE;JIANDAE KUHESABIWA, inalenga katika kuhamasisha ulizni wa watoto ili waweze kusoma kwa bidii ili baadae na wao waje kuwa wabunge na mawaziri.
Maadhimisho haya yalienda sambamba na maadhimisho ya siku ya lishe duniani ambapo tulishuhudia wananfunzi kutoka shule mbalimbali zilizopo Kata ya Mafiga wakinywa uji ambao umechanganywa na mchanganyiko wa lishe mbalimbali.
Post a Comment