Header Ads

DC MURO ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MWANANCHI MMOJA KIJIJI CHA MALUMBI KUUWAWA NA TEMBO.






Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Jerry Muro, amethibitisha kutokea kifo cha Mzee mwenye umri wa Miaka 72 aliyefariki baada ya kujeruhiwa na Tembo Kijiji cha Mlumbi Kata ya Mang'onyi Wilaya ya Ikungi 

Akizungumza na Wananchi waliojitokeza  Kijijini hapo, DC Muro, amesema kuwa tukio hilo  limetokea leo Juni 17,  ambapo tembo 3  wakiwa katika msafara wao walivamia Kijiji cha Mlumbi Kata ya Mang'onyi Wilaya ya Ikungi  na kupelekea kifo cha mtu mmoja ajulikaney kwa jina la MAGHIYA NTUI LIMU mwenye umri wa miaka 72.

DC Muro, baada ya kupokea taarifa hiyo, alifika akiwa na Kamati nzima ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo  ilifika katika eneo la tukio na kutembelea eneo hilo na nyumbani kwa Mzee Ntui na kutoa mkono wa rambirambi kwa familia ya Mzee Ntui.

Aidha, katika kuona suala hilo halitokei tena, DC Muro, amezielekeza mamlaka husika kuanza msako mkali wa tembo hao na kuhakikisha wanaondolewa katika makazi ya watu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.