RC SHIGELA AWAACHIA MTEGO SHULE YA SEKONDARI KINGOLWIRA JUU YA UFAULU WA MTIHANI KIDATO CHA NNE 2022.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, ametangaza donge nono la kutoa fedha kwa wanafunzi na Waalimu wa shule ya Sekondari Kingolwira watakaofanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa 2022.
RC Shigela, ametoa kauli hiyo Juni 08/2022 wakati akizungumza na
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kingolwira katika ziara yake ya kukagua ujenzi
wa madarasa yaliyojengwa kupitia mpango wa UVIKO 19 pamoja na kujionea
maendeleo ya shule hiyo.
“ Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa tangia niwe Mkuu wa
Mkoa, nimeona kwenye taarifa ufaulu wenu mwaka jana tulifanya vizuri ila sio
sana sio mbaya,niwaombe waalimu mjipange vizuri tupunguze ikiwezekana tutoe
sifuri kabisa,mimi kuja kuwapa Milioni 5 kwa waalimu wote jambo ambalo
linawezekana na wanafunzi watakaopata daraja A nitampa laki moja ( 100000/=) kila mmoja na matokeo yakitoka mimi nitakuwa wa
kwanza kuangalia matokeo yenu ya Kingolwira “ Amesema RC Shigela.
Aidha, RC Shigela, amewataka Waalimu hao kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu mzuri wa kuwajengea uwezo wanafunzi wa kidato cha nne ambao taaluma yao ipi chini ili kuweza kupunguza sifuri katika mitihani yao ya Taifa ya mwaka 2022.
Post a Comment