Header Ads

Baraza Maalum la kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali lafanyika Chalinze


Mkuu wa idara ya Fedha na Biashara Ndg. Ponsian Kirumbi.

 ChalinzeDc Yafanya Baraza maalumu la kujadili Hoja za CAG.

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kupitia kwa Baraza lake la madiwani hii leo limefaanya Baraza maalumu la kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ikiwa ni kabla ya kukamilika kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Baraza hilo maalumu la kujadili hoja za Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ilianza kwa kusomwa kwa  ripoti ya Ukaguzi kutoka wa fedha za serikali na Mkuu wa idara ya Fedha na Biashara Ndg. Ponsian Kirumbi kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji.

Mara baada ya ripoti hiyo Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bi.Mary Kiboko ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwakuwa na hati safi inayoridhisha kwa takribani miaka mitatu mfululizo

“Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaipongongeza Halmashauri ya Chalinze kupitia Baraza la madiwani,Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Watendaji wote kwa usimamizi mzuri wa fedha na kuhakikisha Halmashauri inapata Hati safi.

Katika Baraza hilo maalum lililohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa kupata hati safi kutoka katika ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ambapo amepongeza ushirikiano wanauonyesha baina ya waheshimiwa madiwani na watendaji katika kusimamia vyema fedha za serikali na kufanya kazi kwa umoja.

Vile vile Mhe. Kunenge ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze pamoja Halmashauri zote kutengeneza mazingira ya kutoa elimu ya Uchumi kwa Madiwani ili waweze kuibua vyanzo vipya vya Mapato ,kuviendesha pamoja na kutafuta masoko kutoka sehemu mbalimbali.

“Naiagiza Halmashauri ya Chalinze kuwepo kwa mafunzo kwa madiwani wote juu ya masuala ya uchumi yanayohusu ubunifu,kuona fursa na kutafuta masoko na ninataka Mabaraza yote ya  madiwani katika Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kuzungumzia masuala ya uchumi kwani itasaidia kuongeza mawazo ya kuongeza kipato kwa Halmashauri na mikakaki ya kuongeza uchumi wa Chalinze na Mkoa kwa ujumla”Amesema Mhe.Kunenge.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Abdallah ameipongeza Serikali kwa hatua ya  kuipa Bajeti yote ofisi ya CAG kama walivyoomba kwani itaongeza ufanisi kwa ngazi ya Taifa na hata kwa Wilaya kwani wakaguzI wa ndani watakuwa na wigo mpana wa kukagua matumizi ya fedha pamoja na majengo ya serikali.

“Naishukuru na nimefurahishwa na serikali yetu kwa kuipa Bajeti yote kama ilivyoombwa na ofisi ya CAG kwani itasaidia kuongeza ufanisi wa kazi zao na pia ukaguzi utafanyika  kote kwa matumizi ya fedha na pia kukagua muonekano na ubora wa majengo ya serikali na itasaidia kupunguza hoja zisizo za lazima”.Amesema Mhe.Zainabu.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe. Hassan Mwinyikondo amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuwa wako tayari kuungana nae ili kupata elimu na semiana mbalimbali zinazohusu masuala ya uchumi.

“ Naungana na wewe Mhe.Mkuu wa Mkoa na tupo tayari kupata elimu na semina za uchumi hata ikiwa kwa kuchangia ili waletwe wataalamu wazuri kutufundisha uchumi ili vikao vyetu vya madiwani viwe vya kiuchumi Zaidi kuliko kuangalia mapato na matumizi pekee”. Amesema Mhe

Aidha Mhe. Mwinyikondo amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Abdallah kwa kusimamia mapato kwa kuunda vikosi kazi vitatu ili kuweza na kudhibiti upotevu wa mapato.

Lengo la Baraza maalum hilo lilikuwa ni kujadili hoja mbalimbali kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali pamoja na kufanyia kazi mapendekezo yaliopendekezwa na ofisi ya CAG.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.