KILIO CHA MAJI SASA BASI, RC SHIGELA ATOA NENO LA MATUMAINI, MKUNDI, LUKOBE TUNGI KICHEKO.
WAKAZI wa Kata ya Mkundi, Lukobe pamoja na Tungi wapo katika hatua za mwisho wa kupatiwa majibu ya kilio chao cha maji kilichokuwa kikiwakabili kwa muda mrefu.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, wakati wa ziara yake
ya kukagua ujenzi wa Kituo cha kusukuma
maji kilichopo Kata ya Kihonda eneo la Mizani ya zamani kinachosimamiwa na
MORUWASA chini ya Mkandarasi Daino Tech Engineering Ltd Morogoro.
Akizungumza
na Waandishi wa habari katika ziara hiyo, RC Shigela, amesema Mkoa wa Morogoro
licha ya kuwa na vyanzo vya maji lakini bbado wananchi uhaba wa maji ulikuwa
ukitawala kwa kutegemea chanzo kimoja cha Bwawa la Mindu.
RC
shigela,amesema ni wakati sasa wa Wakazi hao kuanza kufurahia matunda ya Rais
Mhe. Samia Suluhu Hassani ya kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya Visima na vituo
vya kusukuma maji vyenye thamani ya Zaidi ya Bilioni 1
“ Haya ni
maeneo mapya hivyo tunatarajia mradi huu ukikamilika utaweza kuwahudumia wakazi
wa Mkundi, Lukobe, na Tungi kwani ujenzi unaendelea kwa kasi na umefikia
asilimia nzuri asilimia 40 na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni
30/2022” Amesema RC Shigela.
Aidha,
amesema mradi wa kisima cha tenki la maji umegahrimu Milioni 600, na kituo cha
kusukuma maji umegharimu milioni 590
wenye pampu 2 na milioni 467 kwa ajili ya tenki lingine litakalo lisha
wakazi wa Kilimanjaro na Tungi.
“ Rais wetu
amedhamiria kumshusha mwanamke ndoo kichwani, Manispaa yetu ya Morogoro
tumeokea kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 700 ambazo tayari zinaendelea
kutumika, hata ule mradi Rais wetu
aliosaini wa Tirioni 1 sisi Morogoro tupo na Mji wetu wa Ifakara wanaenda
kunufaika nao, tunaamini mradi huu utakamilika mwezi Agosti na kilio cha maji
katika maeneo niliyo yataja hapo juu tutakuwa hatuna tena changamoto hiyo ya
maji” Ameongeza RC Shigela.
Naye
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Pascal Kihanga, amemshukuru Rais
Samia Suluhu Hassan, kwa kuwakumbuka Manispaa ya Morogoro kwa kuwapatia fedha
za mradi mkubwa wa maji ambao utaenda kuondoa kilio cha Wana Morogoro ikiwamo
Tungi, Lukobe, Maeneo ya Kilimanjaro Kihonda pamoja na Tubuyu.
Post a Comment