RC SHIGELA APIGA HARAMBEE YA KIBABE UKARABATI WA BARABARA KATA YA MKUNDI, AWATWISHA ZIGO ZITO MBUNGE NA MANISPAA.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro , Mhe. Martine Shigela, amewaahidi wananchi wa Kata ya Mkundi kukarabati barabara za ndani ambazo zimekuwa ni changamoto kupitika hususani katika kipindi cha msimu wa mvua.
Hayo ameyazungumza Mei 31/2022 wakati akihutubia Mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero xa wananchi wa Kata ya Mkundi uliofanyika eneo la mwisho wa stendi ya haisi Mkundi mwisho.
RC Shigela ,amesema imekuwa ni vigumu sana wakati wa mvua gari na wananchi kupita katika barabara hizo hivyo anatafuta njia bora ya haraka ya kuweza kufanya ukarabati wa barabara hizo za ndani ilibarabara hizo ziweze kupitika misimu yote ya mwaka .
Alisema licha ya ukarabati wa barabara hiyo pia usambazaji wa umeme katika maeneo yote ambayo hayana umeme atahakikisha umeme unafika ili kuharakisha maendeleo katika Kata hiyo na maeneo yote yasiyo na umeme katika Mkoa wa Morogoro.
Amesema kwa kuanzia matengenezo hayo atapelekea shilingi
milioni 5 ambapo katika fedha hizo Manispaa ya Morogoro itachangia Milioni 1 na
nusu , Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood atachangia milioni
2 na nusu na Mkuu wa Mkoa yeye atachangia Milioni 1 fedha ambazo zitaelekezwa
kuanza maboresho ya haraka.
Katika ziara zake, Mhe. Shigela, alianza ziara ya kusikiliza
na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Mkundi Mei 31/2022 na kumalizia Kata
ya Kihonda Juni 01/2022.
Post a Comment