JITIHADA ZA RC MOROGORO KUPANDA MITI ZAJIDHIHIRISHA KUPATA TUZO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela (kushoto) kama alama ya kutambua mchango wa Mkoa huo kushiriki kwenye kampeni za upandaji miti. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jaffo. TUZO hiyo imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais lJuni 5 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Shigela akipanda mti .
Hapa Mhe. RC anaongea na wadau mbalimbali wa Mazingira (hawapo pichani). kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga.
.
Mkoa wa Morogoro umejipanga upya kuhakikisha unarejesha Uoto wa asili kupitia Mkakati wa kupanda miti kama sehemu ya kuhifadhi, kutunza na kulinda mazingira ya Misitu ndani ya Mkoa huo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mazingira lililofanyika ukumbi wa Magadu Mess Manispaa ya Morogoro, tukio hilo liliambatana na shughuli ya upandaji wa Miti katika Shule ya msingi ya Magadu kama sehemu ya kutekeleza mkakati huo.
Mikakati iliyopangwa na Mkuu wa Mkoa huo akishirikiana na Viongozi wa chini yake wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, viongozi wengine wa chama na Serikali, ni kuhakikisha taasisi za Serikali zikiwemo shule za Msingi na Sekondari pamoja na wadau wengine kuwa wanapewa miche ya miti kwa ajili ya kupanda na kurejesha uoto wa asili ndani ya Mkoa huo.
Mikakati hiyo ambayo imekuwepo tangu mwaka mmoja uliopita ndio haswa umeaanza kuonesha matokea chanya ya uoto wa asili kuanza kurejea taratibu katika baadhi ya maeneo lakini pia na Serikali kuanza kutambua mchango wake katika kampeni ya Upandaji miti na kutoa TUZO kwa MKoa huo.
Post a Comment