Header Ads

NAIBU MEYA MANISPAA YA MOROGORO AZINDUA DIWANI NDWATA CUP AWAMU YA PILI 2022.

 

Naibu Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwele,(kushoto),akisalimiana na wachezaji wa Timu ya MORUWASA.

Naibu Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwele,(kushoto),akisalimiana na wachezaji wa Timu ya MAN CITY .

Naibu Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwele,(kushoto),akizindua mashindano hayo kwa kupiga penati.

Timu ya MORUWASA.

Timu ya MAN CITY

Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Mhe. Hamis Ndwata akizungumza mara baada ya uzinduzi wa michuano hiyo.

NAIBU Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Sabasaba, Mhe. Mohamed Lukwele,  amezindua mashindano ya Diwani Ndwata CUP 2022 , ambayo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuinua vipaji vya vijana na kuwasaidia kuondokana na matatizo yanayowakumba.

Mashindano hayo, yamezinduliwa katika Uwanja wa Polister Klabu uliopo Kihonda Maghorofani ambapo Fainali inatarajiwa kufanyika Julai 12/2022.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mhe. Lukwele, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwaweka karibu vijana ili waweze kuwa jamii moja kupitia soka, kujenga undugu na uraia na pia kuondokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

“Mashindano haya yanaratibiwa na Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Mhe. Hamisi Ndwata, nampongeza sana kwa ubunifu huu, lakini mashindano haya ni moja ya utekelezaji wa ilani ya CCM,yenye lengo la  kufufua vipaji vya vijana na nawashukuru waratibu na watu wengine ambao wamefanikisha zoezi hili" Amesema Mhe. Lukwele.

Hata hivyo kwa upande wake mwanzilishi na  mratibu wa mashindano hayo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Eng. Hamisi Ndwata, amewataka Vijana kucheza kwa nidhamu na kwa upendo kwani mashindano hayo kwani yanalengo la kubua vipaji vya vijana.

“Hii ni awamu ya pili ya Mashindano haya, mwanzo tulishirikisha timu 6 mwaka 2021 na sasa timu 12 mwaka huu 2022 , Bingwa wa michuano hii atazawadiwa Sh. 200000/= pamoja na Seti moja ya jezi, mshindi wa pili Sh 200,000/= , na mshindi wa tatu Sh.100,000/=" Amesema Eng. Ndwata.

Kwa upande wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Mabula Rashid Rudewa, amempongeza Mhe. Ndwata kwa hatau za kukuza vipaji kwani Morogoro imekuwa ni kitovu cha kuzalisha wachezaji wazuri na bora.

" Nipo hapa kushiriki, nimepata mwaliko , Ndwata ni ndugu yangu na hiki anachokifanya ni moja ya utekelezaji wake katika kukuza michezo, niwapongeze na waratibu wengine pamoja na timu zote zilizokubali kushiriki mashindano haya" Amesema Mhe. Mabula.

Katika mchezo wa Juni 26/2022, Timu ya Man City ilifanikiwa kuifungasha virago Timu ya MORUWASA kwa goli 1-0 kupitia mchezaji Hassan Hamis dakika ya 90 ya mchezo.

Miongoni mwa timu zinazo shiriki michuano hiyo ni MORUWASA, JL ACADEMY, KIBWETILE,NEW NNG,USITAMBIE UJANA, MAGHOROFANI 'A', MAN CITY, WONDER BOYS, JL 'B',MAGHOROFANI 'B', MTI MPESA ,SPIDER.

KUNDI 'A'-MORUWASA,JL ACADEMY',MAN CITY ,WONDER BOYS

KUNDI 'B'  -MAGHOROFANI 'B',SPIDER,NEW NNG, MAGHOROFANI 'A'

KUNDI 'C'-USITAMBIE UJANA,MTI MPESA,KIBWETILE,JL 'B'.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.