Header Ads

NDWATA CUP AWAMU YA PILI KUTIMUA VUMBI JUNI 26/2022.

 





KATIKA  kukuza vipaji vya vijana katika Kata ya Kihonda Maghorofani, Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani , Mhandisi Hamisi Ndwata,yupo mbioni kuendelea na mashindano ya Ndwata CUP awamu ya pili yanayotarajia kuanza kutimua vumbi Juni 26/2022 Siku ya Jumapili  katika Viwanja vya Polister Klabu Kihonda Maghorofani.


Akizungumza kuelekea michuano hiyo, Eng.  Ndwata,amesema mashindano hayo katika awamu hii ya pili, yatashirikisha jumla ya timu 12 kutoka Kihonda Maghorofani na mshindi wa kwanza ataibuka na zawadi nono.


Eng. Nwata, amesema ameanzisha michuano hiyo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 katika upande wa michezo.

Aidha, Eng. Ndwata, amesema kuwa michuano hiyo inalenga  kuwajengea afya wanamichezo, kuwakinga na matendo ya uharifu,wizi, pamoja na kutumiwa madawa ya kulevya .

"Michuano hii ni awamu ya pili, mwaka 2021 tulianzisha michuano kama hii ambayo ilishirikisha jumla ya timu 6 na safari hii tumeongeza timu 6 na kufanya kuwa timu 12 zitakazo shiriki michuano hii, niwaombe Vijana washiriki michuano hii kama furaha, na moja ya kutengeneza njia ya kufikia mafanikio yao , michezo sio uadui, wacheze kwa urafiki zaidi na malengo tupate vijana wazuri wataoweza kuwakilisha Mkoa wetu kama ilivyo ya kawaida ya Morogoro kutoa vipaji vya wachezaji" Amesema Eng. Ndwata.

” Lengo la mashindano haya ni kukuza vipaji vya vijana wetu, Michezo imekua Ajira kubwa Duniani kote hivi sasa, hivyo kama Diwani nimeoana nianzishe mashindano haya ambayo naamini yatatumika kama fursa kwa wachezaji wetu kuweza kupata Timu kubwa zaidi ya hizi walizonazo sasa" Ameongeza Eng. Ndwata.


Amesema katika michuano hiyo, mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Jezi seti 1 na kiasi cha shilingi 200,000/=, mshindi wa 2 atapata shilingi 200,000/= na msihindi wa 3 atapata shilingi 100,000/=.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.