TAS MOROGORO YAMPONGEZA WAZIRI BASHUNGWA KUJENGEA MAZINGIRA RAFIKI WATU WENYE MAHITAJI MAALUM.
CHAMA Cha Watu wenye Ualbino Mkoa wa Morogoro (TAS),kimempongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa kwa hatua ya kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye uhitaji Maalum.
Hayo yamezungumzwa juni 22/2022 na Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Morogoro, Hassan Mikazi, kufuatia Waziri Bashungwa, kuwaagiza Maafisa Elimu wote nchi nzima kuendelea kuijengea jamii uelewa kuhusu upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum na kuboresha miundombinu na mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika shule ili ziwe rafiki kwa wanafunzi wote wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maaalum.
Mikazi,amesema hatua hiyo itawezesha kufanikisha mpango wa Ajira Jumuishi kwa watu wenye mahitaji maalumu na walemavu.
"Nampongeza Waziri Bashungwa kwa kuja na mfumo huu ambao tutaanza kuona matunda ajira jumuishi kwa kuwa sasa watu wenye uhitaji watakuwa wamejengewa mazigira rafiki kuanzia ngazi za chini wakiwa shuleni " Amesema Mikazi.
Aidha, amesema kuwa ,Katika kuona suala la ajira Jumuishi linakuwa ajenda ya watu wenye ulemavu, lazima sasa Walemavu pia wajione nao ni sehemu ya kuchangia maendeleo ya Nchi na kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kujikwamua kiuchumi.
Bashungwa, ameagiza ifikapo mwishoni mwa julai 2022, uundwe mkakati wa kuboresha elimu ili kuongeza namna bora ya utekelezaji wa mitaala nchini katika kuizibainisha changamoto zilizopo na kuleta ufumbuzi wa nini kifanyike sasa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji.
Post a Comment