Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA.

MANISPAA ya  Manispaa ya Morogoro imeadhimisha siku ya mtoto wa Afrika inayoazimishwa Afrika nzima kila ifikapo tarehe 16 Juni lengo ikiwa ni kukumbuka mauaji ya watoto yaliyofanyika huko SOWETO Afrika ya kusini mwaka 1976. Chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990.

Maadhmisho hayo yamefanyika Juni 16/2022 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwembesongo Kata ya Mji Mpya yakiambatana na maandamano.

Akizungumza katika madhimisho hayo, Mstahiki Meya  Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, amesema kuwa maadhimisho hayo ni kukumbuka  Wanafunzi zaidi ya 10,000 waliandamana kupinga elimu duni na ya kibaguzi ya wakoloni ambapo wanafunzi 176 waliuawa katika maandamano hayo na mauaji hayo yalileta majonzi makubwa katika bara la Afrika  na kusababisha kuwepo kwa siku hii ili kupinga vikali ukatili dhidi ya watoto na kuhakikisha wanalindwa na kupatiwa haki stahiki.

Mhe. Kihanga, amesema kuwa siku ya mtoto wa Afrika inawakumbusha watoto hatua ya kijasiri waliyoichukua watoto wenzao huko Afrika Kusini katika kulinda haki zao.

"Siku hii ni siku ambayo imetukumbusha ujasiri wa watoto wa Afrika kusini katika kulinda haki zao, hatua  hiyo imeonesha kuwa watoto wanaweza kuleta mabadilko hata wakiwa na umri mdogo,hivyo siku hii huadhimishwa kwa maslahi mapana na kuwakumbusha wazazi/wazazi,wadau na serikali kushughulikia changamoto zinazowakabili watoto  ipasavyo" Amesema Kihanga.

Aidha, ameishukuru Manispaa ya Morogoro  kwa kuwathamini sana watoto kwa kufanya jitihada katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa na kutekelezwa katika ngazi zote hususani kwa kuchukua  uwamuzi wa kuunda kuunda Mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya mtaa na kata.

Naye Mratibu wa Dawati la Watoto Manispaa ya Morogoro ambaye pia ndiye mratibu wa maadhimisho hayo, Joyce Mugambi,amesema kuwa Manispaa  imeunda kamati za ulinzi na usalama za wanawake na watoto katika kata 29 na kamati hizi zimekuwa zikielimisha jamii juu ya haki za wanawake na watoto pamoja na kuzilinda.

Mugambi, amesema kuwa  watoto wa Manispaa ya Morogoro bado wanapitia changamoto mbalimbali zikiwemo za vitendo vya ukatili wa kimwili,kihisia,kiuchumi na kingono katika mazingira wanayoishi hivyo ameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau kuendelea kukemea vitendo vya dhidi ya watoto na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake,  Regina Mwamba, anayesoma Shule ya Msingi Mafisa A, ameishukuru Manispaa ya Morogoro kwa kuadhimisha maadhimisho hayo huku akiwaomba Viongozi kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na kupata mahitaji yao ikiwamo  fursa ya kusikilizwa,haiki ya kuendelezwa,haki ya kuishi,haki kwa watoto wa kike kupata nafasi ya kushiriki michezo kama ilivyo kwa watoto wakiume na haki yakulindwa.

Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani  mwaka huu 2020  ni "TUIMARISHE ULINZI WA MTOTO ; TOKOMEZA UKATILI DHIDI YAKE; JIANDAE KUHESABIWA" 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.