Header Ads

RC SHIGELA AWAPA KICHEKO WANAWAKE WA KATA YA KINGOLWIRA.

 


MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, ameibua furaha na vicheko kwa wakazi wa Kata ya  Kingolwira Manispaa ya Morogoro mara baada ya kuruhusu huduma bure kwa Wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Vifijo hivyo vimetokea Juni 08/2022 wakati wa mkutano wa RC Shigela wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi , mkutano ulifanyika eneo la Uwanja wa Ofisi ya Kata jirani na Mahakama ya Kingolwira.

Akizungumza na Wananchi hao waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo, RC Shigela alisema katika afya ya wakinamama na watoto wa umri chini ya miaka ni tano ni muhimu kwasababu wakinamama ndio walezi  wa kila siku na watoto ni taifa la kesho.

“ Katika suala la afya ni vyema tukatilia mkazo sana hususani Rais  wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan la kutaka huduma hii itolewe bure hswa kwa Wajawazito na watoto chini ya miaka 5, niwaombe msigeuze vitega uchumi , nendeni mkakae chini muangalie upya namna ya kuliweka hili, tunataka tutekeleza huduma hii kama sera ya afya ya Kitaifa inavyosema, ukidaiwa risiti toa pesa harafu niletee risiti hiyo harafu uone kama huyo mtumishi atabakia katika kazi hiyo” Alisema RC Shigela.

Katika hatua nyengine, RC Shigela , alisema lazima Vituo vya afya na Hospitali wahakikishe wanaweka utaratibu mzuri wa  kuwa  mapokezi sahihi ya wa mama wajawazito ili waweze kupatiwa huduma bora na zinazostahiki.

”Nilirudie hili na kulisisitiza , wakina mama na watoto chini ya Umri wa miaka tano hawatakiwi kulipa gharama yeyote kama alivyo agiza Rais wetu Samia Suluhu Hassan , hiyo ni kwasababu wakina mama wengi wana maisha ya chini sana na pia wanafanya jukumu kubwa la kuongeza taifa letu, kwa vile fedha zinatengwa katika huduma hii sitosikia tenda wakina mama hawa wakilalamika kutozwa fedha “ Amesisitiza RC Shigela.

Miongoni mwa kero zilizosikilizwa na kupatiwa majibu  ni pamoja na  Elimu, Maji, Umeme , Ardhi , Afya , Miundombinu ikiwamo barabara, madarasaja na stahiki za watumishi.

Mwisho, RC Shigela, amewaomba wananchi wa Mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano mkubwa katika zoezi linaloendelea la Anwani za Makazi pamoja na kujiandaa kikamilifu katika zoezi la SENSA linalotarajiwa kufanyika Agosti 23/2022.

Huu ni muendelezo wa ziara zake za Kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ambapo kwa Manispaa ya Morogoro alianza ziara Kata ya Mkundi, Kihonda, Kingolwira na Tungi huku akitarajia kuzifikia Kata zote  29 za Manispaa ya Morogoro .

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.