RC SHIGELA ARIDHISHWA NA UJENZI WA MADARASA YA UVIKO 19 SHULE YA SEKONDARI KINGOLWIRA.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, ameridhishwa na ubora wa ujenzi wa madarasa 4 yaliyojengwa kupitia mpango wa UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Kingolwira Manispaa ya Morogoro.
Kauli hiyo
ameitoa Juni 08/2022 katika ziara yake ya kukagua ujenzi huo alipopita akiwa na
Mkutano wa Kusikiliza na Kutatua kero za Wananchi wa Kata ya Kingolwira.
RC Shigela,
amesema Serikali imeendelea kutekeleza kwa mafanikio makubwa Mpango wa
Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mpambano dhidi ya Ugonjwa wa Visrusi vya
Korona (UVIKO 19) wenye thamani ya Shilingi Trioni 1.3 kwa kuimarisha
upatikanaji wa huduma za jamii ambapo kwa Mkoa wa Morogoro fedha hizo zimeweza
kunufainisha katika Sekta ya elimu na Afya.
Aidha, RC Shigela, ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro kwa
kusimamia
vilivyo hadi kukamilisha kwa wakati miradi hiyo ya ujenzi wa
madarasa
ya fedha za UVIKO 19.
“ Nimeona hapa mmeenda vizuri madarasa yana ubora, pia
niwaopongeze kusimamia miradi hii kikamilifu Rais wetu Samia Suluhu ametuletea
Bilioni 1 na laki 7 na nimeona madarasa 86 mmeyakamilisha vizuri na watoto wetu
wanasoma kwa nafasi na waalimu pia wanafundisha kwa ufanisi mkubwa, kikubwa
Wanafunzi wasome kwa bidii na waalimu wafundishe kwa bidii” Amesema RC Shigela.
Mwisho,
RC Shigela, amewaagiza wakurugenzi kuhakikisha kwamba wanatenga fedha kupitia
mapato yao ya ndani kwa kushirikiana na
nguvu za wananchi kuelekeza nguvu zao katika ujenzi wa matundu ya Vyoo pamoja
na ujenzi wa nyumba za Waalimu ili waalimu waishi jirani shule.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja wa mheshimiwa
Rais samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro idara ya Elimu
Sekondari wamepokea kiasi cha Tsh, 1,720,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 86 vya
madarasa.
Post a Comment