Header Ads

IDARA YA AFYA YAHAKIKISHIWA KUTATURIWA STAHIKI ZAO.

AFISA Utumishi wa Manispaa ya Morogoro, Pilly Kitwana, amewahakikishia watumishi wa Idara ya afya kuwa stahiki zao zote wanazifanyia kazi ili kuleta ufanisi kazini.

Kauli hiyo ameitoa Juni 09/2022 wakati wa kusikiliza na kutatua kero za idara ya afya katika Ukumbi wa Mikutano wa Soko Kuu Chifu Kingalu Morogoro.

“Niwahakikishie kuwa sisi kama maafisa utumishi tutahakikisha kuwa tunasimamia stahiki zenu zote ili muweze kuzipata kwa wakati, hivyo tutaandika barua kwa Katibu Mkuu kuhusu masuala yenu na wote mtapata nakala hiyo ya ufuatiliaji wa stahiki zenu , kikubwa niwaombe tuendelee kufanya  kazi kwa bidii katika utoaji wa huduma kwa wateja wetu kwani suala lenu tunalifanyia kazi kwa ukaribu sana” Amesema Kitwana.

Kitwana,  ameongeza kuwa katika masuala ya ufuatiliaji wa stahiki zao watumishi wote wa idara hiyo wahakikishe vielelezo vyao vinakamilika wanapodai stahiki zao.

Vilevile watumishi  wa idara ya afya  wametakiwa kuhakikisha kuwa wanapohama kutoa kitua kimoja cha kazi kwenda kingine wahakikishe kule wanakohama wanafuatilia stahiki zao ili kurahisisha ulipwaji wa stahiki zao kwa wakati kule wanako hamia.

Wakiongea kwenye kikao hicho, watumishi wa idara ya afya, wamewashukuru Maafisa utumishi Kwa kutenga muda wa kusikiliza kero zao na kuzitolea majibu ambayo yamewatia moyo na kuamsha hali ya utendaji wa kazi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.