MEYA KIHANGA AWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA UADILIFU.
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Morogoro kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu.
Kauli hiyo ameitoa leo Juni 21/2022 katika Jukwaa la
Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Morogoro lililofanyika katika Ukumbi wa Savoy
Morogoro Manispaa.
Akizungumza katika Jukwa hilo, Mhe. Kihanga, amesema
kutofanya kazi kwa kuzingatia uadilifu kuna pelekea ubadhilifu wa fedha pamoja
na migogoro ndani ya ushirika.
“Lazima mfanye kazi kwa uadilifu , msiruhusu migogoro,mkiwa
na migogoro hata wale wanaotaka kutoa misaada hawatawaletea tena, simamieni
miiko ya Uongozi ili Wanachama wenu waweze kunufaika na Ushirika huu” Amesema
Kihanga.
Aidha, Kihanga, amewataka Viongozi kufanya kazi kwa
kusimamia sheria na kanuni badala ya kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo
halitawafikisha mbali na kutofika mafanikio au malengo waliojiwekea.
Hata hivyo, amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika
kuhakikisha katika Mikutano yao agenda kubwa iwe uadilifu ili kujenga uwaminifu
kwa wanachama wao.
Kuhusu changamoto ya vyama vya mazao, amezitaka Taasisi za
kifedha kuvitembelea vyama hivyo na kuweza kutatua changamoto zao.
Naye Mwenyekiti wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Morogoro, Idd
Rajabu, amesema lengo la Mkutano huwa wa Jukwaa la Vyama vya Ushirika ni
kuwakutanisha wana Ushirika na wadau wake kwa ajili ya kujengeana uwezo na
uzoefu ili kujenga Ushirika Imara na
wenye nguvu.
Kwa upande wa Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa
Morogoro, Keneth Shemdoe, amesema kazi kubwa ya kufanya katika kuimarisha Vyama
Vya Ushirika ni kutoa elimu na ushauri, usimamizi na ukaguzi .
Shemdoe ,amesema kuwa katika Mkoa wa Morogoro kuna jumla ya
upungufu wa Maafisa Ushirika 22, hivyo kuna kila haja ya kuweza kupata
wataalamu hao ili kuimarisha vyama hivyo kwa ngazi za Halmashauri.
Mwisho, Shemdoe, amesema kwa sasa jukumu kubwa la Jukwaa la
Vyama Vya Ushirika ni kuimarisha Masoko na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Post a Comment