MWENYEKITI TAS ATOA WITO KWA TAASISI KUSAIDIA WATU WENYE ULEMAVU
MWENYEKITI wa Chama cha watu wenye Ualbino mkoa wa Morogoro, Hassan Mikazi,akizungumza na Wadau.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias akizungumza na wadau.
MWENYEKITI wa Chama cha watu wenye Ualbino mkoa wa Morogoro, Hassan Mikazi, ameziomba taasisi kuhakikisha wanashughulika katika kuwasaidia watu wenye ulemavu kama ili kufikia malengo yao.
Wito huo ameutoa hivi karibuni, wakati wa semina na mafunzo elekezi juu ya mradi wa ajira Jumuishi unaohusisha kada mbalimbali ikiwamo Waandishi wa habari, vyama vya watu wenye ulemavu, Taasisis za Umma na Serikali na waajiri semina ambayo imefanyika katika Ofisi za TAS Mkoa iliyopo Kilakala Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na wadau walifika katika mafunzo hayo, Mikazi, ametoa wito kwa taasisi zingine za Serikali pamoja na na taasisi binafsi kuwakumbuka watu wenye ulemavu kwa kutatua changamoto zao za kila siku hasa pale wanapokuwa katika majukumu yao.
Mikazi amesema miongoni mwa huduma wanazotakiwa kukumbukwa watu wenye ulemavu ni pamoja na kutoa vifaa ambavyo vitaweza kuwasaidia kutatua changamoto ziinazowakabili walemavu pamoja na kuwapa vipaumbele katika shughuli za Maendeleo na kuwajengea mazingira rafiki ya kimiundombinu.
"Niombe ndugu zetu na Mashirika ya Umma na Serikali pamoja na Taasisi kuwa na moyo wa huruma kwa kuwasiaida watu wenye ulamavu kwa kutatua changamoto zao kwa ujumla" Amesema Mikazi.
Pamoja na hayo, Mikazi, ameaomba watu wa usalama kujaribu kutoa elimu kwa baadhi ya madereva hasa katika maeneo ya zebra kuweza kuheshimu alama hizo pale wanapopita watu wenye ulemavu wakivuka barabara.
Kwa upande wa Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ili kuendana na wakati na kutatua changamoto hizo serikali imeanza kupokea maoni kutoka kwa wadau yatakayo saidia kuboresha sera mbalimbali zinahusu kundi hilo.
Internews Tanzania wamekuwa wadau wakubwa ambao ndio wamefadhili mradi huo unaowakutanisha wadau mbalimbali kujadili ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika Nyanja mbalimbali na kutafuta suluhu ya changamoto zinazowakabili.
Post a Comment