WAUMINI WA DINI WAMPONGEZA DIWANI KATA YA MAZIMBU KWA KUSAMBAZA NDOO 30 KATIKA NYUMBA ZA IBADA KWA AJILI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA.
Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, (kulia), akimkabidhi ndoo ya maji na sabuni, mwakilishi wa Msikiti wa Al-Moizo Mazimbu. |
WAUMINI wa dini Kata ya Mazimbu,
wamempongeza Diwani wa Kata hiyo , Mhe. Pascal Kihanga, kwa jitihada za
kuwasaidia Ndoo pamoja na Sabuni kwa ajili ya kunawia katika mapambano ya kujikinga dhidi ya Virusi
vya Ugonjwa wa CORONA.
Wakizungumza kwa yakati tofauti tofauti, kwa upande wa Sheikh wa Msikiti wa Masjid AQSWA,
Sheikh Athumani Msoma, amempongeza Mhe. Diwani kwa jitihada zake za kujikinga
dhidi ya Ugonjwa wa CORONA.
“Tuna mshukuru sana Mhe. Diwani wetu , Pascal Kihanga, kwa kweli
amekuwa karibu sana na sisi katika kila jambo, lakini kikubwa zaidi ameonyesha
ni jinsi gani Serikali ilivyokuwa makini na ugonjwa huu kwa kutuletea ndoo hizi
na sabuni , tunamuhakikishia kwamba tutazidi kutoa elimu kwa waumini wetu ili
kila anayeingia msikitini anawe maji na sabuni lakini kwakuwa utaratibu wetu sisi
Waislamu ni kuchukua udhu ,basi bila shaka na elimu hii tutaelewana wote na
kuiunga mkono Serikali kwa mapambano dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa
CORONA, Serikali imesema tusilete masihala na kweli tunazidi kuliombea Taifa
hili lizidi kuwa katika afya njema na Mwnyezi Mungu inshaallah atatuepushia
mbali kama wote tutatekeleza taratibu za Wataalamu bila kuingiza imani zetu”Amesema
Sheikh Msoma.
Naye Mchungaji wa Kanisa la TGRC Mazimbu Barakuda, Jailos
Maloda, amesema kitendo alichokifanya Diwani wa Kata ya Mazimbu kinapaswa
kuigwa na kuchukuliwa kama kiongozi aliyejitoa kwa ajili ya Wananchi wake.
“Tunamshukuru sana
Mhe. Diwani wetu kwa kuonyesha moyo wa kipekee sana, hatujategemea kama
atafanya jambo kama hili, tumeona baadhi ya maeneno yakifanyika lakini katika
nyumba zetu za ibada tumekuwa tukijitegemea wenyewe kununua vifaa hivi, niseme
kuwa kuungwa mkono na Serikali ni jambo jema sana,Kanisa letu lina milango minne
baada ya kuingia ugonjwa huu, tuliamua kutumia milango miwili amabayo ndiyo
tuliyokuwa tumeweka ndoo na kuwalazimisha waumini kupita huko , sasa ametuongezea
ndoo nyengine tunatarajia ibada yetu ya kesho na kuendelea milango yote itafunguliwa na kupitika”Amesema Mchungaji Maloda.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema kuwa, lengo la kusambaza
ndoo hizo katika Nyumba za ibada imetokana na maeneo hayo kuwa na watu wengi na
elimu ya kujikinga inaweza kusambaa kirahisi.
Amesema katika utafiti wake amegundua kwamba kwenye Nyumba
za ibada ndio kuna watu wengi ambapo hiyo ndiyo sababu iliyomsukuma kuelekeza
ndoo katika mmaeneo hayo.
Miongoni mwa nyumba za ibada zilizosambaziwa ndoo hizo ni
pamoja na Misikiti na Makanisa yote yaliyopo ndani ya Kata ya Mazimbu ikiwa na
lengo la kuwasaidia waumini wa dini kujikinga na Virusi vya Ugonjwa wa CORONA.
“Nimeona nianze na Nyumba za ibada, ukinagalia kwa haraka haraka utagundua kwamba huku kuna watu wengi sana ambao wengine wanakwenda kanisani na
Misikitini lakini bado ni Wananchi wangu , kama Serikali inavyosema haina dini,
nimeona ni vyema nikapitia miskiti yote pamoja
na Makanisa yote yaliyopo katika Kata yangu ili kuyapa nguvu na kuyaunga mkono
katika mapambano ya vita dhidi ya Ugonjwa wa CORONA, najua wengine walishaanza kuchukua hatua za kujikinga lakini kama Diwani wao ni jambo la faraja sana kuona kwamba nina kuwa bega kwa bega na Wananchi wangu hususani katika nyumba hizi za ibada , raia yangu kwamba hivi vifaa tuvitumie na nyie
Viongozi wa dini najua jinsi gani mnavyoguswa na gonjwa hili, endeleeni kutoa
elimu kwa waumini wenu hadi pale gonjwa hili litakapoteketea, tuzidishe maombi
katika kuliombea Taifa letu na Viongozi wetu wanaopambana kila uchwao katika
kujikinga dhidi ya Maambukizi ya Ugonjwa huu wa CORONA”Amesema Mhe. Kihanga.
Aidha, amewataka wananchi kutodharau ushauri wa Wataalamu
badala yake waendelee kuchukua jitihada mahususi za kujikinga na Ugonjwa huo
hadi pale mambo yatakapo kaa sawa na kama kuna mtu atajigundua ana viashiria
vya Ugonjwa huo apige simu kwa wataalamu kama walivyotoa maelekezo ili hatua za
awali ziweze kuchukuliwa.
Katika hatua nyengine, Mhe. Kihanga, amesema anatambua yapo
maeneo mengi yana shida lakini ameanza na Nyumba za ibada na ataendelea
kufanya hivyo katika maeneoe mengine kadri inavyobidi lengo ni kuhakikisha
Wananchi wa Kata yake wanakuwa na uelewa mpana sana juu ya kujikinga na Ugonjwa
CORONA pamoja na usalama wa afya zao.
Pia hakuishia katika Nyumba za ibada pekee, Mhe. Kihanga ameamua
kusambaza Ndoo hizo kwa Viongozi wote wa Serikali za Mitaa walio katika Kata
yeke akidai kuwa wao wamekuwa wakiwahudumia wananchi kila uchwao.
Pia kwa nafasi aliyokuwa nayo ya Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Morogoro, amemuunga Mkono Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, kwa kuweka
Ndoo moja nje ya Geti la kuingilia katika Ofisi ya Manispaa yenye kuonyesha
ndoo hiyo na udhamini wake kama kiongozi wa Manispaa na kujali afaya za
Wananchi wake.
Post a Comment