'Marufuku ujenzi bila kibali' Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro.
Baadhi ya Vibanda vilivyojengwa bila mpangilio na kukiuka masharti ya kibali cha ujenzi. |
Nyumba iliyopakana na mwekezaji unaodaiwa kuwa na utata.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,ametoa onyo kwa Mwananchi yeyote wa Manispaa ya Morogoro kuanzisha ujenzi bila ya kuwa na kibali cha ujenzi.
Onyo hilo amelitoa leo Machi 11,2020, mara baada ya kutembelea katika Mradi wa Hoteli ya Kisasa unaendelea na ujenzi uliopo maeneo ya Stendi ya Mabasi Msamvu ambapo jengo hilo ni mali ya mwekezaji Mbunge wa Jimbo la Gairo, Mhe.Ahmed Shabiby baada ya mipaka kati ya jirani yake kuwa na mzozo.
Amesema kuwa , eneo hilo liliibuka mzozo na mwekezaji huyo kufuatia mwananchi aliye jirani na mpaka huo kukiuka masharti ya kibali cha ujenzi na kujenga kiholela.
Baada ya kupokea malalamiko hayo, Mkurugenzi alimpa agizo mwananchi aliyejenga kinyume na kibali cha ujenzi kwamba hadi kufikia tarehe 28, Machi awe ameviondoa vibanda hivyo au ajenge kutokana na ruhusa ya kibali kinavyosema la sivyo akishindwa atamuagiza Afisa Ardhi kwenda na greda kwa ajili ya kuvibomoa vibanda hivyo.
"Nimeletewa malalamiko na mwekezaji Mhe. Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby akidai kwamba aliyekuwa jirani yake kuna changamoto ya kujenga bila mpangilio, baada ya kufuatilia tuligundua kwamba huyo mtu aliomba kibali cha ujenzi lakini kosa lake ni kwamba badala ya kujenga kama kibali kilivyomtaka yeye akaweka mabanda yasiyo na mpangilio yanayo ondoa taswira nzuri ya eneo hilo ambalo lipo barabarani kabisa,hivyo nimemwambia hadi kufikia tarehe 28 mwezi Machi mwaka 2020, awe amerekebisha na kuweka kama kibali kinavyotaka lasivyo kufikia tarehe 27 bado vibanda vipo nitamugaiza afisa Ardhi aende na greda kwa ajili ya kuvibomoa" Amesema Sheilla.
Katika hatua nyengine, amuagiza Afisa Ardhi kuweka alama ya X katika ujenzi wowote unaoendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ambao hauna vibali vya ujenzi huku akisema jambo hilo halikubaliki na sheria inaruhusu kubomoa nyumba za aina hiyo.
Aidha , amesema kuwa Serikali haina mpango wa kubomoa nyumba za wananchi isipokuwa wanatakiwa kujenga kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha ujenzi.
Naye Afisa Ardhi wa Manispaa ya Morogoro, Gilbert Msemwa, amesema kuwa mtu yeyote anayejenga mjini mahali popote bila kufuata utaratibu wa kumilikishwa yaani kiwanja ambacho hakijapimwa, hajamilikishwa, hana kibali cha wenye mamlaka ya mji unaohusika ujue anajipeleka kwenye hatari ya kuvunjiwa na kuondolewa jengo lake.
"ni marufuku kuwabariki watu waliojenga kwa kuvunja sheria bila vibali,serikali yetu imedhamiria kupunguza na kuondoa migogoro kwa wananchi waliojenga kiholela na kupima maeneo yote ambayo hayajapimwa, kwahiyo Sheria haijasema pembezoni mwa mji watu wajenge tu, sasa usiendelee kujenga na kama umejenga anza sasa kumwambia fundi wako aache kujenga na ujenzi hadi upate kibali.” Amesema Msemwa.
Post a Comment