MANISPAA YA MOROGORO YANUNUA PIKIPIKI 7 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 23 KWA AJILI YA KATA ZA PEMBEZONI.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, akiwasha Pikipiki katika hafla fupi ya makabidhiano ya Pikipiki hizo kwa Kata zilizopo Pembezoni mwa Manispaa ya Morogoro. |
Watendaji wa Kata zilizopo pembezoni mwa Manispaa ya Morogoro wakiwa katika Pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa katika Ofisi ya Manispaa ya Morogoro. |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imenunua Pikipiki saba
(7) aina ya YAMAHA zenye thamani ya Shilingi Milioni 23,100,000/= pamoja na
kodi (VAT) kupitia fedha za Mradi wa kuboresha Miji (ULGSP) katika bajeti ya
mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya kuwajengea uwezo Watumishi kwa kuboresha
utendaji kazi wao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya makabidhiano hayo ya Pikipiki ,Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema Pikipiki hizo
zimenunuliwa Mahsusi kwa ajili ya Kata
za Pembezoni ambazo kwa wakati huu Pikipiki nne
(4) wamwpatiwa Kata za Luhungo, Mzinga , Mkundi pamoja na Kingolwira.
Amesema Pikipiki tatu (3) zimebakia Ofisi Kuu ya Manispaa ya
Morogoro kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Halmashauri.
“Tunaipongeza sana Manispaa kwa kuwa na jicho la tatu
kununua Pikipiki hizi, Kata hizi za pembezoni zinachangamoto sana haswa kwa
Watendaji wake wanashindwa kuwafikia Wananchi kwa urahisi na kushindwa kuitoa
huduma lakini kwa hiki walichokifanya kitatoa
mwanya mzuri wa Watendaji kuwahudumia wananchi wao ipasavyo, lakini niwaombe na
kumuomba Mkurugenzi wetu wa Mansipaa kwamba Pikipiki hizi zitumike katika muda
wa kazi baada ya hapo wewe mtendaji
endelea na mambo yako mengine weka chombo hicho nyumbani kwani isijekuwa
Manispaa imefikiria kuleta maendeleo harafu maendeleeo hayo yakegeuka Vifo
tunajuana tabia zetu sasa tuvileinde na kuvitahamini”Amesema Mhe. Kihanga.
Hata hivyo amewataka Watendaji wa Kata hizo, kuvitumia
vyombo hivyo vya Moto kwa malengo yaliyokusudiwa na sio kuvitumia kwa ajili ya
kugeuza kuwa Bodaboda na kujipatia kipato kwa atakaye kiuka utaratibu
atachukuliwa hatua za Kisheria .
Katika hatua nyengine, amewapongeza Wataalamu wa Manispaa na
kuwaomba mara baada ya Miradi iliyopo kukamilika waanze kufikiria miradi mipya
kwani anaamini Bajeti ijayo ya Mwaka wa fedha wa 2021/2022 Manispaa itakuwa na
fedha za kutosha na kuweza kuwa na bajeti kubwa ya kihistoria.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla
Lukuba, amesema Manispaa imetoa Pikipiki hizo kwa ajili ya kurahisisha huduma
kwa Wananchi na kuhakikisha huduma bora zinapatikana katika Kata hizo.
Amesema kuwa
matarajio yake ni kuona kuwa Pikipiki hizo zinarahisisha kwa kiasi
kikubwa utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Serikali kwani ahata maeneo
yasiyofikika kwa urahisi kwa gari sasa yatafikika.
“Tuvitunze vyombo hivi, Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini
ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
imeonyesha moyo wa kuthamini kazi zetu nasi tuvipe heshima na kuvitumia kwa
malengo tarajiwa, tusiende kuvigeuza Bodaboda na tutawekea utaratibu Yule ambaye
atakiuka utaratibu huu tutamchukulia hatua kazi za kisheria niwaombe Watendaji
chapeni kazi tuendelee kuwahudumia Wananchi wetu katika Utekelezaji wa Ilani ya
Chama Cha Mapinduzi CCM katika kufikia adhima ya Tanzania ya Viwanda na Uchumi
wa Kati”Amesema Sheilla.
Aidha, Mkurugenzi amewataka Watumishi wote wa Manispaa
kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo na kutoa huduma bora kwa
Wananchi.
Post a Comment